Kwa picha: Maua mazuri yapamba dirisha la kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s) na lanukia harufu ya utukufu wake na uaminifu wake…

Maoni katika picha
Maandalizi ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Abulfadhil Abbasi (a.s), ambaye alizaliwa tarehe nne Shabani na kuzaliwa kwa miezi ya Muhammadiyya (a.s), dirisha la kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s) limepambwa maua mazuri yanayo nukia harufu ya utukufu, uaminifu na ikhlasi yake, limekua na muonekano ambao unaongeza furaha katika nafsi za mazuwaru kufuatia tukio tukufu la kuzaliwa kwake.

Upambwaji wa kaburi hili ni moja ya maandalili yaliyo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kusherehekea minasa ya mwezi wa Shabani ambayo itahitimishwa na kumbukumbu ya kuzaliwa kwa muokozi wa walimwengu Imamu wa Zama Msubiriwa (a.f) mwezi kumi na tano Shabani, maua mazuri ya aina mbalimbali yamepangwa juu ya dirisha la kaburi, miongoni mwa maua hayo ni: (Anturiyam, Kalad, Waridi za Holandi, Kalayuul, Rozi, Daudi, Kamiliyaan, Jori, Saksi) pamoja na aina nyingine nyingi.

Kuna maua zaidi ya (3000) yamewekwa katika vyombo vya mapambo (68) sehemu ya juu na chini ya dirisha tukufu, na maua mengine ya wima yapatayo (8) yamewekwa kwenye kaburi tukufu, pambo (sega) la shahabu lililopa sehemu ya kuelekea katika haram tukufu limewekewa maua nane kila upande na maua mawili yamewekwa katika mlango wa kuingia ndani, maua hayo yana vitu maalumu vinavyo yafanya yakae muda mreru bila kuharibika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: