Kamati ya maandalizi ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada awamu ya kumi na nne yatangaza matokeo ya shindano la tafiti…

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la kimataifa na kitamaduni Rabiu Shahada awamu ya kumi na nne linalo andaliwa na kusimamiwa na uongozi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, imetangaza matokeo ya shindano la kitafiti la kongamano litakalo anza Ijumaa ya mwezi tatu Shabani (1439h) sawa na (20 Aprili 2018m) chini ya kauli mbiu isemayo: (Tumepigana kwa utukufu wa Imamu Hussein (a.s) na tumeshinda kwa utukufu wa fatwa).

Mjumbe wa kamati ya maandalizi Shekh Ammaar Hilali amesema kua: “Tafiti zilizo shiriki katika shindano zinakaribia hamsini, zinazo husu mada zilizo tangazwa kushindaniwa, tafiti zote zimefanyiwa uchambuzi na kupimwa kielimu, hatimaye tafiti tano zikaibuka na ushindi, shindano la mwaka huu lilikua na ushindani mkubwa sana.

Shekh Hilali akafafanua kua: “Baada ya matokeo ya mwisho washindi walipangwa kama ifuatavyo:

Mshindi wa kwanza: Dokta Haazim Twaarish Haatim kutoka Iraq, utafuti wake unasema: (lugha ya matangazo ya Zainabiyya katika kupambana na ukandamizaji wa kimataifa – falsafa ya habari).

Mshindi wa pili: Ustadh Abdulqaadir Yusufu Zarnani kutoka Lebanon, utafiti wake unasema: (Uzuri na ubaya wa lugha za khutuba za jihadi).

Mshindi wa pili: “waligongana”: Shekh Hassan Isaawi kutoka Iraq, utafiti wake unasema: (Misingi ya Ashura na nafasi yake katika malezi ya kiharakati ya matashi ya jihadi).

Mshindi ya tatu: Dokat Muhammad Naanaa kutoka Iraq, utafiti wake unaitwa: (Fatwa iliyo badilisha misingi ya nguvu.. utafiti wa athari zake na matokeo yake)

Mshindi wa tatu “wamegongana” Dokata Mustwafa Jafari kutoka Iraq, utafiti wake unasema: (Athari za fatwa ya sasa katika kusahihisha uwelewa mbaya wa hadithi tukufu).

Mwisho wa maongezi yake akasema kua: “Tunakusanya tafiti hizi na kuziongezea mambo muhimu katika maktaba na kuziunganisha na tafiti za miaka ya nyuma”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: