Hivi karibuni kituo cha kuhuisha turathi kilicho chini ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimetoa kitabu cha (Mjulishaji wa zuhudi ya Mtume –s.a.w.w-), ambacho kimeingizwa katika orotha ya toleo lake liitwalo (Mtiririko wa turathi zilizo toweka) ambalo lina muda tangu lianze kutolewa.
Toleo hili limeandikwa na Shekh Jafari bun Ahmadi bun Ali Qummiy (miongoni mwa wanachuoni wa karne ya nne hijiriyya) na likakusanywa na kupangiliwa na Shekh Abdulhalim Audhu Hilliy, na kimepitiwa na kuwekwa faharasi na kituo cha kuhuisha turathi kilicho chini ya Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya.
Hili ni toleo la tatu miongoni mwa matoleo ya mtiririko wa (turathi zilizo toweka), ambazo zilitoweka na kubakia nakala zake zimesambaa katika vitabu mbalimbali, toleo hili ni miongoni mwa vitabu muhimu sana vinavyo mzungumzia Mtume (s.a.w.w), katika kitabu hiki kuna riwaya za wanachuoni wazito kama vile: Sayyid ibun Twausi (aliye kufa 664 hijiriyya) na Shekh Ali Twabarasiy (aliye kufa karne ya 7 hijiriyya), na Allamah ibun Fahdi Hilliy (aliye kufa 841 hijiriyya). Kimekusanywa na kupangiliwa na Shekh Abdulhalim Audhu Hilliy (d.t).