Maonyesho ya vitabu ya kimataifa yapokea wadau wake, na wayasifu kua yana kitu kipya tofauti na maonyesho ya miaka ya nyuma…

Sehemu ya watembeleaji wa maonyesho
Watembeleaji wa maonyesho ya vitabu ya kimataifa yanayo fanyika Karbala awamu ya kumi na nne, ambayo ni sehemu ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu shahada litakalo anza siku ya Ijumaa ijayo –Inshallah- ambao ni watu wa dini, watu wa sekula, watafiti na wadau mbalimbali, wamesema kua maonyesho haya yana kitu kipya na ni mazuri ukilinganisha na maonyesho ya miaka ya nyuma, katika maonyesho haya kuna washiriki wa sekta muhimu kama vile (vituo rasmi vya usambazaji wa vitabu vya tiba, vitabu vya sheria, vitabu vya uchumi na vinginevyo) uwepo wa vitabu hivyo umetoa fursa kwa wanafunzi wa sekula na udaktari kutembelea vituo hivyo moja kwa moja kwa sababu vina mambo yanayo hitaji.

Akaongeza kusema kua: “Hakika maonyesho haya yamekua mazuri kutokana na kuwepo kwa vitabu vya aina mbalimbali, vya dini, tamaduni, jamii na vinginevyo, Ataba mbili tukufu kupitia maonyesho haya zimefanikiwa kuvutia watu mbalimbali, jambo linalo upa mji wa Karbala nafasi ya kua kinara wa kueneza mtazamo wa kitamaduni”.

Kumbuka kua maonyesho haya ni sehemu ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu shahada awamu ya kumi na nne, jumla ya nchi saba zinashiriki ambazo ni (Lebanon, Iran, Jodan, Sirya, Misri, Uingereza na Iraq), vikundi vya usambazaji wa vitabu na taasisi zaidi ya (133) zinashiriki katika maonyesho haya, uongozi wa maonyesho ulihakikisha upatikanaji wa aina mbalimbali za vitabu vinavyo lenga watu wa tabaka zote katika jamii, kuanzia watoto, familia, wanaume, wanawake, vitabu vya kisekula, vya kidini, vya udaktari na vinginevyo, kila aina ya fani ambayo mtu atahitaji kutafuta kitabu chake basi atakipata katika maonyesho haya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: