Vitalu vya Alkafeel vya ingia katika msimu wa Rabii vikiwa na zaidi ya miche milioni moja na nusu ya aina mbalimbali…

Maoni katika picha
Vitalu vya Alkafeel chini ya kitengo cha utumishi cha Atabatu Abbasiyya tukufu vina zaidi ya miche milioni moja na nusu ya aina mbalimbali, ikiwemo miche ya msimu, ya kudumu, ya kivuli pamoja na miche ya matunda, hili halikutokea kwa bahati mbaya, bali limetokana na mipango na utendaji wa idara ya vitalu pamoja na uwezo wa wataalamu wake, ambao wana uzowefu wa kufanya kazi hiyo, kutokana na utendaji wao mzuri wamefanikiwa kuwa na idadi kubwa ya aina mbalimbali ya miche huku mingine ikiwa imeingia kwa mara ya kwanza katika ardhi ya Iraq.

Kiongozi wa vitalu vya Alkafeel Ustadh Muayyad Haatif Muhammad ameuambia mtandao wa Alkafeel ulipo tembelea vitalu vya kijani kua: “Vitalu vya Alkafeel vina sifa moja kubwa, sio vitalu vya msimu na havina miche michache au aina fulani tu, ni vitalu endelevu katika kipindi chote cha mwaka, lakini kipindi cha Rabii ni kipindi muafaka cha kupanda mimea na kupendezesha bustani, tunaingia katika msimu huu tukiwa na miche milioni moja na nusu ya aina mbalimbali, sehemu kubwa ya miche hiyo imeandaliwa ndani ya vitalu vyetu (kwa kupandikiza miche au kupanda mbegu) baada ya kufanyiwa majaribio ilikua na matokeo mazuri, na tumeweza kuepuka, kuagiza miche nje ya nchi ambayo ndio njia inayo tumiwa na vitalu vingi”.

Akaongeza kusema kua: tulijikita katika aina za miche zifuatazo (za kudumu, za msimu na za kivuli) zikiwemo (Batunia, Qahwaan, Yaldaz, Jicho la paka, Mapambo, Qadifa, Jafariy, Istur malakiy, Kazania, Madhfuru, Ilyaas mazhar, Haidar dhilliy, Banjaminiyya, Akasiya Misriyya, Akasiya Fistula na aina zingine nyingi nafasi haitoshi kuziandika zote, hali kadhalika vitalu vya Alkafeel vinazalisha (Thayyil) ya Holandi ambayo inaongoza kwa kijani kibichi wakati wote masika na kiangazi”.

Akaendelea kusema: “Uongozi wa vitalu vya Alkafeel umeaandaa zaidi ya vitalu (5000) vyenye aina mbalimbali za miche kama vile (Machungwa, Lanki, Naumi Baswar, Naumi Halo, Naumi Haamidh, Sindi, Karibu Furut, Naranji) hali kadhalika tuna vitalu vyenye aina mbalimbali za mimea na vina sifiwa na kila mtu”.

Akasema: “Hakika watumishi wa vitalu vya Alkafeel wanafanya kazi kwa ratiba maalumu kutokana na aina ya miche wanayo hudumia kama ni ya kudumu au ya msimu pia wana miche inayo kubaliana na hali ya hewa ya Iraq, miche yao wanauza kwa bei nafuu ambayo raia yeyote wa Iraq anaimudu”.

Mwisho wa maneno yake Ustadh Muayyad alitoa wito kwa watu wote watembelee vitalu na wajionee kile wanacho zalisha, tunajiandaa na kupanda miti na maua barabarani na maeneo ya umma kwa bei nafuu sana ukilinganisha na bei ya kuagiza nje, pia aina za miti na maua yetu inaendana na hali ya hewa ya taifa hili.

Kwa kuwasiliana na watumishi wa vitalu vya Alkafeel unaweza kufika katika kituo chao kilichopo katika mkoa wa Karbala barabara ya Husseiniyya karibu na jengo jeupe au piga simu zifuatazo (07724830002 au 07718003738).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: