Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel inaendelea kutoa mafunzo kwa wanachama wake…

Maoni katika picha
Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel chini ya idara ya watoto katika kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, inaendelea kutoa mafunzo ya Skaut kila siku ya Ijumaa kwa kipindi cha mwaka mzima, ispokua kipindi cha mitihani ya shule kwa wanachama wake wenye umri wa miaka 7 hadi miaka 18 wapatao (140) mara mbili kwa siku asubuhi na jioni, ambapo hutumia jumla ya saa 4 hadi 5 katika mafunzo kwa siku.

Hufundishwa mambo mbalimbali ambayo ni (elimu ya dini, utamaduni, mazowezi na michezo) kwa kufuata ratiba iliyo andaliwa na jumuiya, hakika mafundisho hayo yanafaida kubwa kwa washiriki, pia hufanyika mashindano ya michezo kwa ajili ya kuwajenga zaidi kimichezo na kuwafanya wajitambue uwezo wao, hali kadhalika kuna ratiba ya kutembelea sehemu takatifu za kidini na maeneo ya makumbusho na kihistoria, na kuweka mahema maalumu ya Skaut.

Kufanyika kwa mafundisho haya kunatokana na jinsi Atabatu Abbasiyya tukufu inavyo thamini kujenga uwezo wa watoto na vijana pamoja na kuendeleza vipaji vyao kwani wao ndio msingi wa taifa la kesho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: