Kutokana na kuingia mwezi mtukufu wa Shabani…. Kuta za Atabatu Abbasiyya tukufu zapambwa kwa maua mazuri…

Maoni katika picha
Furaha na shangwe vimeenea katika ukumbi wa haram tukufu ya Abbasi (a.s) kwa ajili ya kuupokea mwezi mtukufu wa Shabani na kuhuisha kuzaliwa kwa miezi mitukufu ya Muhammadiyya (a.s), kuta za Atabatu Abbasiyya pamoja na nguzo zake zimepambwa kwa maua mazuri yanayo ashiria furaha za waumini, kwa nini wasifurahi wakati wanasherehekea kuzaliwa kwa waombezi wao na safina ya uongofu Maimamu waongoaji baada ya Mtume (s.a.w.w).

Kiongozi wa idara ya ukumbi wa haram, wa kitengo cha usimamizi wa haram bwana Jaasim Muhammad Kaadhim ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: Kitengo kimekamilisha maandalizi yote yanayo hitajika katika upambaji wa haram na kuweka maua pamoja na kutengeneza majukwaa yatakayo tumika katika sherehe hizi tukufu.

Akaongeza kusema kua rangi za vitambaa vilivyo wekwa katika ukumbi na ambavyo vimeandikwa ujumbe unao onyesha utukufu wa tukio hili, ilichaguliwa kwa kushauriana na idara ya ushonaji katika kitengo cha zawadi na nadhiri cha Ataba tukufu, kawaida rangi zinazo ashiria furaha hutofautiana na rangi zinazo ashiria huzuni.

Ijumaa ya kesho ambayo ni tarehe 3 Shabani 1439h, ni kumbukumbu ya kwanza ya mazazi katika mwezi huu wa Shabani, nayo ni siku ya kuzaliwa kwa bwana wa vijana wa peponi Imamu Hussein (a.s).

Tunapenda kuwafahamisha kua kesho ni siku ya ufunguzi wa kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu shahada awamu ya kumi na nne, litakalo funguliwa ndani ya ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s) na baadhi ya vipengele vya kongamano hilo vitafanyika ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: