Kukamilika maandalizi ya kongamano la wanawake la nane pembezoni mwa kongamano la Rabiu shahada awamu ya kumi na nne.

Maoni katika picha
Kamati kuu inayo simamia kongamano la wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kukamilika kwa maandalizi ya kongamano hilo, ambalo ni sehemu ya kongamano la Rabiu shahada awamu ya kumi na nne.

Rais wa kamati kuu ya maandalizi Ustadhat Bushra Kinani amesisitiza kua; kongamano la mwaka huu litapendeza zaidi ya miaka ya myuma, kwani kamati zote za maandalizi (kamati ya matangazo, uhusiano, utumishi, Qur’an…) zimekamilisha maandalizi kwa muda ulio pangwa, chini ya usimamizi wa moja kwa moja wa kamati kuu.

Akafafanua kua, kongamano hili litakua na ushiriki wa nchi kumi, ambazo ni: (Algeria, Gini, Saudia, Bahrain, Oman, Iran, Swiden, Ufilipino, Norway), kongamano la mwaka huu litakua na vipengele mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kikao cha usomaji wa Qur’an katika siku ya ufunguzi, na igizo pamoja na filamu inayo elezea harakati za idara ya wanawake na kaswida na mashairi.

Akaongeza kusema, jambo lingine katika kongamano la mwaka huu kutakua na warsha maalumu ya kujadili matatizo ya familia yaliyo zungumzwa na Marjaa, ambayo ni ongezeko la talaka na mpasuko wa familia, chini ya watalamu walio bobea katika elimu ya nafsi na sheria za dini…

Hali kadhalika kutakua na kubadilishana uzowefu pamoja na wageni waliokuja kutoka nje ya Iraq, kuhusu sekta ya habari, utamaduni, familia, maendeleo ya binadamu pamoja na sekta ya Qur’an.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: