Msafara wa Alwafaa wa kibinadamu uliofanywa na kikosi cha Abbasi cha wapiganaji umetangaza kukamilisha program zake.
Kiongozi mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, Ustadh Maitham Zaidi alibainisha katika mkutano wa kuhitimisha program hizo ulio fanyika katika upande wa kulia wa mji wa Mosul: “Hakika kipawa mbele chetu kikubwa ni kudumisha mawasiliano na familia za mashahidi pamoja na majeruhi kutokana na kujitolea kwao na tunakusudia kufika kila sehemu ya nchi yetu kipenzi na katika mikoa yote”.
Akaongeza kusema kua: “Msafara huu umefanya kazi mbalimbali katika mji wa Mosul, kitengo cha wahandisi kimefanikiwa kufungua barabara zaidi ya kumi upande wa kulia wa mji wa Mosul, pia wameifanyia matengenezo barabara ya Badushi – Tal-afar, aidha wamekarabati shule na wamesafisha kituo cha maji cha Badushi”.
Akaendelea kusema: “Msafara wa Alwafaa umekaa siku 6 katika mji wa Mosul na wamefanya kazi saa 116, wamefanya vikao 100 ambavyo wamekutana na taasisi za kiraia, za ulinzi na usalama, familia za mashahidi na zenye kuishi katika mazingira maumu, hatukukutana na kiongozi yeyote wa kisiasa au mgombea wa uchaguzi, hali kadhalika tulikutana na ndugu zetu wa kabila la Zaidiyya katika mji wa Ba’shiqah, Hazani na Sanjaar, pia tulikutana na watu wa tabaka tofauti miongoni mwa wakazi wa mkoa wa Nainawa”.
Akafafanua kua: “Msafara wetu ulihusisha miji mingi ya Nainawa, kama vile: (Bartwala, Ba’shiqah, Hazani, upande wa kulia, Upande wa kushoto, Badushi, Tal-afar, Sanjaar na miji mingine mingi)”.
Akasisitiza kua: “Msafara ulifikia malengo yake yote, tulikutana na watu wote tulio kusudia kukutana nao, ispokua ndugu zetu katika wakfu sunni, walikua na majumu mengine yaliyo zuia kukutana nao, tulikua tumekusudia kuanza kusaidia uandaaji wa malalo na mazaru ambapo kuna mambo yanayo hitaji ushirikiano”.
Akaashiria kua: “Tunatamani umoja wa mataifa uweke ofisi yake katika mji wa Nainawa kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa mji huo, sisi tutafungua ofisi yetu katika mji wa Nainawa na haita fungwa hadi kazi ya mwisho itakapo isha, ofisi hiyo itaongozwa na vijana wa Mosul”.
Akabainisha kua: Kama sio fatwa tukufu ya Marjaa dini mkuu, magaidi wa Daesh tusinge washinda, nao ni hatari kwa taifa na ulimwengu mzima, walimwengu ni wadeni wa kujitolea kwa wairaq, tunapenda kusema kua Msafara wa Alwafaa unahaki ya kupata msaada kutoka katika serikali ya Iraq na wizara ya ulinzi na kutoka kwa uongozi mkuu wa Hashdi Sha’abi, Atabatu Abbasiyya ndio mlezi mkuu wa Msafara huu mtukufu.
Akamaliza kwa kusema kua: Zaidi ya taasisi hamsini na wanaharakati pamoja na vyombo vya habari wametangaza kujiunga na msafara huu, tunatoa wito kwa taasisi za kitaifa na kimataifa zijiunge na msafara huu, hatupokei msaada wowote wa pesa taslim, bali tunahimiza msaada huo wapewe moja kwa moja wahitaji, tupo tayali kusaidia taasisi yeyote ya kimataifa katika upande wa ulinzi na usalama na kuhakikisha wanatekeleza malengo yao.
Tunapenda kusema kua; Msafara wa Alwafaa umeundwa kwa kuzingatia vigezo vya kibinadamu kwa ajili ya kutoa misaada katika mikoa tofauti ya Iraq na tumeanza na mikoa ya kusini kisha itafuata mikoa ya kaskazini na hatimaye tuenee katika mikoa yote ya Iraq.