Jioni ya Alkhamisi –usiku wa Ijumaa- mwezi tatu Shabani, mwaka wa nne hijiriyya, alizaliwa mjukuu wa pili wa Mtume (s.a.w.w) Imamu Hussein (a.s), Mtume (s.a.w.w) akampokea akiwa na furaha, huku bishara ya kuzaliwa kwake ikiwa imeenea mbinguni na ardhini.
Alhamuwini anasema kwa sanadi ya ibun Abbasi: Wakati alipo zaliwa Hussein bun Ali (a.s), Mwenyezi Mungu alimuambia Malaika mlinzi wa moto, azime moto kwa ajili ya heshima ya mtoto wa Muhammad aliye zaliwa duniani.
Baada ya kuzaliwa alichukuliwa na babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) akamuweka kifuani kwake na akambusu, kisha akamuadhinia katika sikio la kulia na akamkimia katika sikio la kushoto na akampa jina la Hussein kwa amri ya Mwenyezi Mungu mtukufu, na akamfanyia hakika ya mbuzi, akamuambia mama yake Fatuma (a.s), mnyowe kichwa chake na utowe sadaka ya fedha kwa uzito wa nywele zake, Mtume (s.a.w.w) akamuwekea mate yake matukufu katika kinywa chake, husemwa: alimfanyia hakika ya mbuzi na akatoa sadaka kwa uzito wa nywele zake tukufu, zilikua na uzito wa dirham.
Mtume (s.a.w.w) alisimamia maleli yake yeye mwenyewe na alionyesha kumjali sana, ikachanganyika roho yake na yake na upole wake na wake, akawa ni kopi yake na mtu atakaye endeleza malengo yake na kulinda misingi yake, Imamu Hussein (a.s) alifanana na babu yake Mtume (s.a.w.w), alifanana naye katika sifa na katika umbo, alikua ni mbora kushinda mitume wote.
Hussein na ndugu yake Hassan (a.s) walikulia katika mikono mitukufu ya mama, baba na babu, walikula chakula safi kutoka kwa babu yao Mtume (s.a.w.w), akawarithisha adabu yake na ushujaa wake, jambo lililo muandaa (Hussein) kubeba majukumu makubwa ya Uimamu baada ya baba yake na kaka yake Mujtaba (a.s), Mtume (s.a.w.w) aliongea kuhusu Uimamu wao katika sehemu nyingi, Mtume anasema: (Hassan na Hussein ni Maimamu wawe wamesimama au wamekaa).
Hakika alifuata nyayo za Utume na Uimamu, alikua na utukufu na kimaumbile na kinasaba, Hussein (a.s) alikua ni kopi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika umati wake, anatembea katika mwongozo wa Qur’an tukufu na anaongea kwa kufuata fikra za ujumbe wa Muhammadiyya na anafuata mwenendo wa babu yake, na anabainisha tabia njema na kusimamia matatizo ya umma, haghafiriki kuongoza umma na kuunasihi na kuunusuru, yeye mwenyewe akawa ni mfano hai kwa yale wanayo takiwa na sheria, alikua ni nuru ya uongofu kwa walio potea.. na kinywaji kitamu kwa wanao kipenda.. na nguzo muhimu kwa waumini.. na hoja inayo tegemewa na watu wema, na kielelezo cha haki wanapo tofautiana waislamu.. na upanga wa uadilifu ambao Mwenyezi Mungu anakasirika na kufurahi kutokana nao.
Abu Abdillahi Hussein (a.s) ana nafasi kubwa ambayo haifikiwi na yeyote zaidi ya baba yake, mama yake, kaka yake na maimamu watakatifu watokanao na kizazi chake (a.s), katika kubainisha nafasi ya Imamu Hussein (a.s), kuna aya nyingi ndani ya Qur’an tukufu zinazo elezea utukufu wake, miongoni mwa aya hizo ni: Aya ya Tatwihiir, iliyopo katika surat Ahzaab, aya ya 33, Aya ya Mubahala, katika surat Aal-Imraan, aya ya 61, na katika surat Shuura, aya ya 23, na zinginezo nyingi.
Imamu Abu Abdillahi Hussein bun Ali bun Abu Twalib (a.s) Shahidi wa Karbala, wa tatu katika Maimamu wa Ahlulbait (a.s) na bwana wa vijana wa peponi kwa makubaliano ya wana hadithi wote, mmoja wa watoto wawili walio endeleza familia ya Mtume (s.a.w.w) na mmoja ya watu wanne walio chukuliwa na Mtume (s.a.w.w) kwa ajili ya kwenda kuapizana na manasara wa Najrani, na ni miongoni mwa watu wa kisaa (walio funikwa shuka) na Mwenyezi Mungu akawaondelea uchafu na akawatakasa, pia ni miongoni mwa watu wa karibu ambao Mwenyezi Mungu ameamrisha tuwapende, na mmoja wa wale ambao atakaye shikamana nao ataokoka na atakaye wahalifu atapotea na kuangamia.