Kwa ushiriki wa zaidi ya vituo na taasisi (133) kutoka katika nchi saba: Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zafungua awamu ya kumi na nne ya maonyesho ya vitabu ya kimataifa Karbala…

Sehemu ya ufunguzi
Kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Hussein (a.s) na miongoni mwa vipengele vya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu shahada, asubuhi ya leo siku ya Ijumaa (3 Shabani 1439h) sawa na (20 Aprili 2018m) umefanyika ufunguzi rasmi wa maonyesho ya vitabu ya kimataifa awamu ya kumi na nne kwa ushiriki wa zaidi ya vituo na taasisi (133) kutoka katika nchi saba ambazo ni: (Uingereza, Lebanon, Iran, Misri, Jodan, Sirya na Iraq) yanayo fanyika katika eneo la uwanja wa katikati ya haram mbili lililo pauliwa.

Ufunguzi wa maonyesho haya ulihudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na katibu wake mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar pamoja na katibu mkuu wa Atabatu Husseiniyya tukufu Sayyid Jafari Mussawi, na jopo kukwa la viongozi wa Ataba mbili tukufu, pamoja na mwakilishi wa vituo vya usambazaji na taasisi zinazo shiriki katika maonyesho haya, na wageni wa kongamano la Rabiu shahada litakalo anza jioni ya leo chini ya kauli mbiu isemayo: (Tumepigana kwa utukufu wa Imamu Hussein (a.s) na tumeshinda kwa utukufu wa fatwa).

Watu walio shiriki katika ufunguzi huo waliingia katika korido za maonyesho hayo na wakashuhudia kinacho onyeshwa, maonyesho haya yamehusisha vitabu vya aina tofauti vinavyo lenga tabaka zote za watu katika jamii, kuanzia watoto hadi wazee wanaume kwa wanawake wasomi wa dini na wa sekula, bali kila aina ya fani utapata kitabu chake.

Mjumbe wa kamati ya maandalizi Sayyid Aqiil Abdulhussein Yasiri amesema kua: “Maonyesho ya mwaka huu yana nchi nyingi washiriki na aina mbalimbali za vitabu, kuna vitabu vya kisekula, kidini, vitabu vinavyo husu watoto na kila aina ya elimu utakayo hitaji, tumeona dalili za kuridhika kwa watu wanao tembelea maonyesho haya kutokana na uzuri wa mpangilio wake pamoja na uzuri wa eneo yanapo fanyika, ambapo ni katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, kila mtu ameridhika na eneo hili”.

Mkuu wa maonyesho haya Dokta Mushtaqu Ali ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hakika maonyesho haya ni sehemu ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu shahada awamu ya kumi na nne, zimeshiriki jumla ya nchi saba, ambazo ni: (Lebanon, Iran, Jodan, Sirya, Misri, Uingereza, pamoja na mwenyeji wao Iraq), jumla ya vituo vya usambazaji na taasisi (133) zimeshiriki katoka katika nchi hizo, uongozi unao simamia maonyesho haya ulihakikisha yanakua na aina tofauti za vitabu vinavyo lenga tabaka zote za watu katika jamii”.

Kumbuka kua maonyesho ya vitabu ya kimataifa ni moja ya sehemu za kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu shahada linalo simamiwa na kugharamiwa na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya tangu kuanzishwa kwake miaka kumi na nne iliyo pita, ambalo ni sehemu ya kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: