Balozi wa Holandi nchini Iraq ameonyesha kufurahishwa kwake na makumbusho ya Alkafeel, kutokana na vitu vilivyomo ambavyo historia yake inarudi miongo kadhaa ya nyuma, na ni kumbukumbu muhimu za kihistoria, pia ameridhishwa na mpangilio mzuri wa maonyesho hayo.
Hayo yalitokana na ziara aliyo fanya balozi huyo katika Atabatu Abbasiyya tukufu na kutembelea makumbusho ya Alkafeel ya vifaa na nakala kale, katika matembezi hayo alifuatana na wasimamizi wa maonyesho ambao walimuelezea vitu vilivyomo ndani ya makumbusho, alikua anasimama kwa muda mrefu katika vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na sehemu ya mabaki ya kubba tukufu la haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) lilipo shambuliwa kutokana na maandamano matukufu ya Shaabaniyya.
Alipongeza juhudi zinazo fanywa na wasimamizi wa idara ya makumbusho, akasema kazi yao inasaidia kufungua akili na fikra, akaushukuru uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kutilia umuhimu jambo hili tangu mwanzo.
Mwisho wa ziara yake balozi aliagwa kwa bashasha kama alivyo pokelewa, huku akisifu juhudi zinazo fanywa na watalamu wa makumbusho ambao wameyapangilia vizuri na kuyafanya yawe na vigezo vya makumbusho ya kimataifa.