Mwaka wa kumi na nne mfululizo na katika ardhi ya utukufu Karbala ndani ya ukumbi wa haram ya malalo ya Imamu Hussein (a.s), Alasiri ya leo mwezi tatu Shabani (1439h) sawa na (20 Aprili 2018m) zimeanza program za kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu shahada awamu ya kumi na nne, linalo simamiwa na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Hafla ya ufunguzi imehudhuriwa na wasomi wa dini na wa sekula kutoka ndani na nje ya Iraq, pamoja na wawakilishi wa Ataba mbalimbali na mazaru tukufu za Iraq na nje ya Iraq, pamoja na wawakilishi wa serikali ya mkoa wa Karbala na Najafu na idadi kubwa ya mazuwaru na wageni waalikwa, bila kusahau vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa, washiriki wa kongamano hili wanatoka katika nchi zaidi ya (30) za kiarabu na kiajemi.
Hafla ya ufunguzi itapambwa na uwasilishwaji wa ujumbe wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, pamoja na ujumbe wa uongozi wa wakfu Shia, sanjari na ujumbe kutoka kwa wageni washiriki na vipande vya mashairi.