Mwakilishi wa ujumbe wa bara la Afrika katika kongamano la Rabiu shahada: Ushindi mkubwa mlio upata wairaq ni ushindi wa binadamu wote dhidi ya maadui zao…

Maoni katika picha
Shekh Shabani Liyon –mbunge wa zamani-, Imamu, khutibu na mwalimu katika kituo cha Rasuli Akram katika nchi ta Madagaska amesisitiza kua, ushindi mkubwa walio upata wairaq ni ushindi wa binadamu wote dhidi ya maadui zao, aliyasema hayo katika ujumbe alio wasilisha kwenye hafla ya ufunguzi wa kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu shahada lililo anza Alasiri ya Ijumaa (3 Shabani 1439h) sawa na (20 Aprili 2018m) kwa niaba ya ujumbe wa bara la Afrika, miongoni mwa aliyo sema ni:

“Tunafuraha sana kwa kupata mwaliko wenu na kuja kushiriki pamoja na nyie tukiwa pamoja na ndugu zetu kutoka kila sehemu ya dunia, tuna sherehekea pamoja kuzaliwa kwa bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s), tumekuja kutoka katika nchi yetu kipenzi kisiwa cha Madagaska hadi katika ardhi takatifu ya Karbala, ardhi ya bwana wa mashahidi (a.s) mwenye msimamo wa uislamu na ubinadamu halisi, aliye jitolea kila kitu kwa ajili ya islahi ya umma wa babu yake Mtume Muhammad (s.a.w.w)”.

Akaongeza kusema kua: “Mwaka huu tunasherehekea pamoja na nyie kuzakiwa kwa bwana wa mashahidi (a.s) sambamba na kusherehekea na kuwapongeza kwa kukomboa ardhi yote ya Iraq kutoka kwa magaidi, na ushindi wa Iraq katika vita dhidi ya dhulma na ugaidi”.

Akamalizia kwa kusema: “Ushindi huo mtukufu ulianzia sehemu hii, ilipo tolewa fatwa tukufu ya Mheshimiwa Sayyid Ali Sistani, iliyo pelekea mwaka huu tuweze kusherehekea ushindi huu, ambao ni ushindi wa ubinadamu dhidi ya maadui wake, kwa mara ya pili tunashukuru wito wenu kwetu wa kuja kushiriki katika kongamano hili, tunaomba iwe sababu ya kuendeleza mawasiliano pamoja na nyie vile vile pamoja na ndugu wote walio kuja kutoka kila nchi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: