Barua iliyo sainiwa na familia za mashahidi ikienda kwa Mheshimiwa Marjaa mkuu Sayyid Ali Sistani…

Maoni katika picha
Hafla ya ufunguzi wa kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu shahada lililo anza leo mwezi tatu Shabani (1439h) sawa na (20 Aprili 2018m) ilihitimishwa kwa kusoma barua iliyo sainiwa na familia za mashahidi walio kufa kwa ajili ya kuilinda Iraq na raia wake pamoja na maeneo matakatifu, walio itikia mwito wa Marjaa dini mkuu katika mji wa Najafu Ashrafu.

Ifuatayo ni nakala ya barua hiyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.

Mheshimiwa mtukufu Marjaa mkuu Sayyid Ali Sistani.

Kila sifa njema anastakimi Mola mlezi wa walimwengu na rehma na amani ziwe juu ya Muhammad na Aali zake watakatifu, Mwenyezi Mungu anasema katika kitabu chake titukufu, Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu (..Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi wa mahala pakuweka ujumbe wake..) Amesema kweli Mwenyezi Mungu mtukufu.

Tunaweka mikono yetu katika maneno haya huku tukiamini kua wewe ni baba yetu na baba ya umma mzima, wala hatutarajii kupata heshima kubwa zaidi ya kuitwa watoto wako kutokana na jinsi unavyo jali mazingira halisi kwa kuzingatia sehemu na muda, kwa namna ulivyo pambana na hatari iliyo ikumba nchi yetu kipenzi Iraq na malalo matakatifu ya watu wa familia ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) na maeneo yote matakatifu, ulitoa fatwa tukufu iliyo jaa baraka, ikaja kuokoa taifa na umma kwa ujumla kutokana na njama za kishetani, Mwenyezi Mungu alifelisha njama zao na hawakupata ispokua aibu na hasara, kutokana na mwitikio wa umma huu, walishindana wazee kwa vijana kuitikia mwito mtukufu (wa jihadi ya kujilinda) na ndipo baba zetu na ndugu zetu wakaandika historia ya ushindi kwa damu zao takatifu kwa ajili ya kuhami dini na taifa lao kipenzi, wakaonyesha uaminifu na mapenzi kwa Abu Abdillahi Hussein (a.s) kwa kuinusuru haki, uliwakusudia wao pale ulipo sema maneno yako matukufu yaliyo jaa huruma na upole ambayo hatuwezi kuongeza kitu, ukawasifu na kutoa pole kwa kusema: miongoni mwa daraja ndogo zaidi ya kuwatendea wema mashahidi watukufu walio mwaga damu zao tukufu katika ardhi ya Iraq ni kusaidia familia zao mayatima na wajane, na sisi tunahuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Hussein (a.s) kwa utukufu wa fatwa yako na utukufu wa damu zilizo mwagika, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awarehemu mashahidi wetu na awaponye haraka majeruhi na awaneemeshe wapiganaji wetu kwa kuwapa ushindi na aendelee kutunufaisha pamoja na waislamu wote kwa kukupa umri mrefu.

Wa salaamu alaikum wa rahmatu llahi wa barakaatuhu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: