Mwezi nne Shabani ulimwengu ulinawirika kwa kuzaliwa Mwezi wa bani Hashim…

Maoni katika picha
Mwezi nne Shabani ni siku aliyo zaliwa Abulfadhil Abbasi mtoto wa kiongozi wa waumini (a.s) aitwaye Mwezi wa bani Hashim na muasisi wa utukufu, ulimwengu ulinawirika kwa kuzaliwa Mwezi wa bani Hashim na nuru yake ikaangaza utukufu, akanyonya maziwa ya ushujaa na akalelewa na miguu ya ukhalifa, akapata ushujaa na utukufu pamoja na kuipa nyongo dunia. Kuzaliwa kwa Abulfadhil Abbasi (a.s) kulikua sawa na mawalii wengine wa Mwenyezi Mungu, kulikua na bishara nyingi zilizo ashiria utukufu wa mtoto anaye zaliwa mbele ya Mwenyezi Mungu.

Imamu Amirulmu-uminina (a.s) kabla ya kuzaliwa kwa Abbasi (a.s), bali kabla hata ya kumuoa mama yake Ummul Banina, alielezea sifa zake, aliashiria kua atakua shujaa na mwenye imani imara, mwenye nafsi nzuri, mwenye moyo imara, mwenye tabia njema na kwamba atamuhami ndugu yake Imamu Hussein (a.s) kwa nafsi yake, na atatoa kila alicho nacho kwa ajili ya ndugu yake, na atafia katika ardhi ya Karbala mbele ya ndugu yake.

Kuzaliwa kwake: Mtoto wa kwanza wa mama mtukufu Ummul Banina ni Abulfadhil Abbasi (a.s), dunia ilinawirika kwa kuzaliwa kwake, familia ya alawiyya ikaingiwa na furaha kwa kuzaliwa Mwezi wao ulio iangazia dunia utukufu wake, Amirulmu-uminina (a.s) alipo pata habari ya kuzaliwa mtoto huyu mtukufu, alikwenda haraka nyumbani kwake akamchukua na kumbusu, akamuadhinia katika sikio lake ya kulia na akakimu swala katika sikio lake ya kushoto, sauti ya kwanza iliyo penya katika masikio yake ilikua ni sauti ya baba yake jabali la imani na ucha Mungu hapa duniani, sauti iliyo kua ikisema “Allahu Akbaru…” hadi “Laa ilaaha illa Llah”. Maneno hayo matukufu ambayo ndio ujumbe wa Mitume yakamwingia Abulfadhil Abbasi (a.s), kisha Amirulmu-uminina (a.s) akamnyoa na akatoa sadaka ya dhahabu au fedha kwa uzito wa nywele zake, akawapa masikini, na akamfanyia hakika kwa kuchinja mbuzi, kama alivyo fanya kwa Hassan na Hussein.

Kupewa kwake jina: Imamu Amirulmu-uminina (a.s) alimpa jina la (Abbasi) mwanaye, na alikua anajua kua atakua shujaa miongoni mwa mashujaa wa kiislamu, atakua chukizo kwa kila mtu muovu na mwenye kufanya batili, na atamfurahisha kila mwenye kufanya mema, hakika alikua kama alivyo bashiriwa, alikua chukizo kwa kila adui aliye wapiga vita Ahlulbait (a.s), aliwashinda majemedari wao, alieneza hofu ya kifo kwa maadui wote katika vita ya Karbala, mshairi anasema:

Nyuso za maadui zilijaa hofu ya kifo, huku Abbasi akiwa ni mwenye kutabasamu na kucheka.

Umbo lake: Hakika alikua na sura nzuri sana, hadi alipewa jina la laqabu (sifa) la Mwezi wa bani Hashim kutokana na uzuri wa sura yake, na mwili wake ulikua umejaa na unamuonekano wa ushujaa na nguvu, alikua na msuli wa nguvu na mwenye sura nzuri, alikua mrefu kiasi akipanda juu ya farasi mkubwa miguu yake inakanyaga chini.

Hakika Abulfadhil alikua na kila aina ya utukufu, alikua mfano wa pekee katika utiifu na kunufaika na ndugu yake Imamu (Hussein ambaye ni bendera ya islahi) yeye na ndugu yake Shahidi (a.s) ni kielelezo cha ta-awili ya kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo (Naapa kwa jua na mwanga wake na mwezi unapo chomoja), alinufaika na kila kauli ya Imamu au kitendo bali kila kitu kilicho fanywa na Imamu yeye alikua mtu wa kwanza kusoma kwake na kukifanyia kazi, alimfuata na kumtii ndugu yake katika kila kitu hadi katika tarehe za kuzaliwa, Imamu kazaliwa mwezi tatu Shabani na yeye kazaliwa tarehe nne mwezi huo huo mwaka wa ishirini na sita hijiriyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: