Wageni kutoka nchi (33) washirikiana na watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwake…

Maoni katika picha
Wageni kutoka nchi (33) mashariki na magharibi ya dunia, walio kuja katika kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu shahada awamu ya kumi na nne wanashirikiana na watumishi wa Abulfadhil Abbasiy (a.s) katika kusherehekea siku ya kuzaliwa kwake ambayo ilikua ni tarehe nne ya mweni mtukufu wa Shabani.

Tukio hili limefanyika siku ya pili ya kongamano, wageni hao walipo simama bega kwa bega na watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wakiwa wamebeba maua na kuelekea katika kaburi tukufu, program ilianza kwa kusomwa Qur’an tukufu na ziara ya Mwezi wa bani Hashim (a.s) halafu ukaibwa wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu.

Program hii imehudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmad Swafi na katibu mkuu Muhandisi Muhammad Ashiqar, pamoja na wawakilishi wa Atabatu Husseiniyya na Askariyya tukufu. Wahudhuriaji wote pamoja na watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu walisoma kwa pamoja ziara ya Abulfadhil Abbasi (a.s) sambamba na wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu.

Tunapenda kukumbusha kua, program hii kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi mkuu wa kisheria aliyo toa siku za nyuma, alisema kua: “Hakika watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s), leo wanasimama kutoa salam, ambayo inawakilishwa na vitendo ambavyo ni sehemu ya kuonyesha uaminifu kwa Abulfadhil Abbasi (a.s), ambalo ni jambo muhimu kushinda kutoa maneno au kusoma beti za mashairi, hakika inatakiwa kujikita katika kufanya kazi zaidi kwa ajili ya kuenzi utukufu wa mwenye malalo hii takatifu, pia ni ukumbusho kwa watumishi wa eneo hili kua wanafanya kazi sehemu tukufu na kinacho takiwa kwao ni ushindi tu, kila mtu anaye simama sehemu hii tukufu hatakiwi kufikiria kushindwa, akishindwa atakua kapata hasara, kila mahala katika sehemu hii inaongea haki”.

Wageni wa gongamano walionyesha kufurahishwa kwao na kisimamo hiki, kwani ni kusimama mbele ya kamanda wa kiislamu, Shekh Abduljalil Issa Naawi kutoka Marekani amesema kua: “Kwa hakika sina maneno ninayo weza kuelezea furaha yangu na hisia nilizo nazo kwa kusimama sehemu hii tukufu ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kufanya ibada hizi, japo kua nimesha kuja zaidi ya mara moja sehemu hii lakini mara hii ni ya pekee kabisa, kwa sababu inasadifu tarehe za kuzaliwa kwa miezi ya Muhammadiyya (a.s), nawashukuru sana wasimamizi wa kongamano hili na wasimamizi wa program hii”.

Baada ya hapo ukafanyika ufunguzi wa sistim ya sauti katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ambayo ni sistim ya kisasa zaidi na yenye uwezo mukubwa ukilinganisha na iliyopo sasa, ni miongoni mwa sistim bora za kimataifa, kisha baada ya hapo wakaenda kutembelea makumbusho ya Alkafeel ya vifaa na nakala kale.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: