Miongoi mwa ratiba ya siku ya pili (4 Shabani 1439h) sawa na (21 Aprili 2018m) ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada awamu ya kumi na nne, jioni ya Juma Mosi kimefanyika kikao cha usomaji wa Qur’an ndani ya haram tukufu ya Husseiniyya katika mazingira yaliyo jaa furaha kufuatia kumbukumbu ya mazazi yaliyo tokea ndani ya mwezi huu mtukufu wa Shabani.
Sayyid Ali Abudi Twaaiy kutoka katika kituo cha ufundishaji wa Qur’an cha Darul-Qur’an ya Atabatu Husseiniyya tukufu amesema kua: Hakika hafla hii hufanywa kila mwaka, ni miongini mwa vipengele vya kongamano la Rabiu Shahada, na hushiriki katika usomaji, wasomi wakubwa wa Qur’an wa kimataifa, washiriki walio soma mwaka huu wametoka Indonesia na katika Atabatu Radhawiyya tukufu pia hapa Iraq.
Walio soma ni (Bwana Osama Karbalai kutoka Iraq, na Sayyid Fadhlani Zainu-Dini kutoka Indonesia, pamoja na mkuu wa Darul-Qur’an katika Atabatu Radhawiyya tukufu Shekh Mahdi Shujaa), hao ndio walio burudisha masikio ya wahudhuriaji kwa kuwasomea Qur’an tukufu, na mwisho wa program hii wakasoma washiriki wa mradi wa mahafidh elfu moja, unao simamiwa na Darul-Qur’an ya Atabatu Husseiniyya tukufu, pamoja na vijana wenye umri mdogo walio hifadhi Qur’an nzima kwa namba za aya na kurasa.
Katika ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kulifanyika kikao cha usomaji wa mashairi, ambacho walishiriki washairi kutoka mikoa tofauti ya Iraq, alianza mshairi kutoka Karbala bwana Qassim Bakhiit, kisha kutoka Baabil bwana Muhammad Faatwimiy, baada yake akasoma mwana Ali Fatalawi kutoka Waasit, halafu akafuata mshairi kutoka Karbala bwana Alaa Baibwai, ukafuata mkoa wa Naswiriyya, akasoma bwana Hussein Habthaliy, halafu akasoma bwana Alaa Isaawi kutoka Basra, ukafuata mkoa wa Samawa, akasoma bwana Hassan Barakiy na mwisho kabisa akasoma mshairi kutoka Karbala bwana Zainul-Aabidina Saidi.