Mbele ya kaburi tukufu la Imamu Hussein (a.s) wawakilishi wa nchi (33) waitikia wito na wafanya ziara…

Sehemu ya ziara
Kutoka katika haram ya Abu Abdillahi Hussein (a.s) kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mwanaye Imamu Sajjaad (a.s), na miongoni mwa ratiba ya siku ya tatu ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu shahada awamu ya kumi na nne, wageni wa kongamano siku ya Juma Pili (5 Shabani 1439h) sawa na (22 Aprili 2018m) wamefanya program ya kiibada pamoja na watumishi wa Atabatu Husseiniyya tukufu, iliyo hudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai pamoja na katibu wake mkuu Sayyid Jafari Mussawi, sambamba na ugeni ulio wakilisha Atabatu Abbasiyya tukufu ulio ongonzwa na katibu mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar.

Program hiyo ilianza kwa kusomwa Qur’an tukufu na bwana Aadil Karbalai, kisha ulifuata ukaribisho ulio fanywa na muongoza hafla Ustadh Haidari Salaami, alianza kwa kukaribisha wageni na akatoa pongezi kwa Mitume na Maimamu watakasifu (a.s), pamoja na Maraajii wa dini ya kiislamu na waislamu wote kwa ujumla kutokana na kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Miezi ya Shaabaniyya, ambapo siku kama ya leo alizaliwa Imamu Sajjaad (a.s).

Baaada ya hapo ilifuata program ya usomaji wa Qur’an tukufu, ambayo walishiriki wanafunzi watatu wa mradi wa mahafidh elfu moja unao simamiwa na Atabatu Husseiniyya tukufu, program hiyo iliendeshwa kwa njia ya maswali na majibu, wageni wa kongamano walikua wanauliza maswali kuhusu namba ya aya, ukurasa ilipo, jina la sura na kama ipo mwanzo, katikati au mwisho wa ukurasa, na wanafunzi hao walikua wanatoa majibu.

Kisha kwa unyenyekevu mkubwa na utulivu, wahudhuriaji walielekea katika kaburi tukufu la Abu Abdillahi Hussein (a.s) wakasoma ziara maalumu kwa ajili yake (a.s) halafu wakaendelea kufanya ibada ndani ya haram hiyo tukufu.

Mazingira tulivu ya kiibada yaliacha athari kubwa kwa washiriki wa program hii, rais wa klabu ya waarabu amesema kua: “Nilipo simama mbele ya Abu Abdillahi Hussein (a.s) nilipata hisia zisizo elezeka, kutokana na utukufu wa eneo hili takatifu, kwa hakika hisia hizi nilizo zipata hapa hazipatikani mahala pengine, nitawaambia jamaa zangu mazingira ninayo ishi katika siku hizi, ambayo wao pia wanahitaji kua katika mazingira haya, natamuni salamu hizi zifike kila nchi hapa duniani”.

Naye Ustadh Jawaad Ghauk mwanachama wa umoja wa wanachuoni wa Jaafariyya nchini Uturuki alisema kua: “Utukufu ulioje kusimama pamoja na kundi hili mbele ya Abu Abdillahi Hussein (a.s), nimesha kuja mara nyingi katika Ataba hizi za Iraq lakini sikuwahi kupata hisia kama nilizo pata katika program hii, na nimeirekodi katika simu yangu, kwa muda mfupi tu watu walio ifuatilia wamefika elfu 44, nawashukuru sana waandaaji wa kongamano hili kwa kutupa nafasi ya kuja kushiriki, natamani tuendelee kushiriki kila mwaka”.

Kumbuka kua kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Husseiniyya tukufu, Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai amesha wahi kuongea kuhusu program hii kua: “Hakika inasaidia kuwajenga watumishi wa Abu Abdillahi Hussein (a.s), kutengeneza uhusiano wa kiibada baina ya kiumbe na Muumba, na kumfanya afungamane naye wakati wote, program hii inahusisha kusoma ziara ya Imamu Hussein (a.s) na dua, na hufanywa kila siku, kupitia vitu hivyo husaidia kuingiza katika akili ya mtumishi wa sehemu hii, nafasi ya Imamu Hussein (a.s) na kwa namna gani alipata daraja kubwa kiasi hiki, ziara hii imetaja sifa alizo kua nazo bwana wa mashahidi (a.s), miongoni mwa sifa hizo ni, jihadi, subira, kuamrisha mema na kukataza mabaya, hali kadhalika inajenga misingi ya uhusiano na kuingiza hisia za hadhi ya Imamu Hussein (a.s) katika nafsi ya mtumishi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: