Kikao kilifunguliwa kwa Qur’an tukufu, ahalafu ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, na kiliongozwa na Dokta Khaalid Adnaan Hassan, aliye elezea kwa ufupi tafiti tatu za:
- 1- Dokta Abdulqaadir Yusufu kutoka Lebanon, utafiti wake unasema: (Khutuba za kidini baina ya misimamo mikali na ya kawaida.. khutuba za jihadi kwa mfano).
- 2- Shekh Fadhili Jazaairiy kutoka Aljeria, utafiti wake unasema: (Kanunu za Mwenyezi Mungu na tatwa tukufu).
- 3- Dokta Muhammad Na’naa Hassan kutoka Iraq, utafiti wake unasema: (Fatwa iliyo badilisha viwango vya nguvu – utafiti wa athari zake na matokeo yake).
Kikao hiki kilishuhudia umakini wa tafiti ambazo hazijawahi kufanywa hapo kabla, na zilipata mwitikio mkubwa, pia wahudhuriaji walitoa michango yao na maoni yao pamoja na kuuliza maswali, na mwisho watafiti wakapewa zawadi.