Baada ya kupita siku mbili za vikao vya kitafiti: Kuhitimishwa kwa vikao hivyo katika kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu shahada awamu ya kumi na nne…

Maoni katika picha
Ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu Alasiri ya Juma Pili (5 Shabani 1439h) sawa na (22 Aprili 2018m) ulishuhudia kuhitimishwa ka vikao vya kitafiti vya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu shahada awamu ya kumi na nne, kwa ushiriki wa watafiti kutoka ndani na nje ya Iraq, walio wasilisha mada za kidini na kisekula, na kuhudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, na katibu wake mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar, pamoja na ujumbe ulio wakilisha Atabatu Husseiniyya tukufu ukiongozwa na katibu wao mkuu Sayyid Jafari Mussawi na jopo kubwa la wageni wa kongamano walio furika ukumbini hapo.

Baada ya Qur’an ya ufunguzi na kusomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wema wa Iraq, kikao cha mwisho cha utafiti kilifunguliwa na kuongozwa na Dokat Mushtaqu Ali ambaye alielezea mihtasari ya tafiti nne zifuatazo:

  • 1- Utafiti wa Shekh Abdulhalim Shirara kutoka Lebanon usemao: (Baina ya mwenendo wa Husseiniyya na fatwa ya Sistaniyya, msisitizo wa mwenendo (mwema) na kuhami umma).
  • 2- Utafiti wa Shekh Abdullahi Dishti kutoka Kuwait usemao: (Khutuba za kidini baina ya msimamo mkali na wa kawaida).
  • 3- Utafiti wa Shekh Najmu-Dini Twabasi kutoka Lebanon usemao: (Khutuba za Ashura na athari yake katika kuendelea kukubalika kwa fatwa tukufu ya kujilinda).
  • 4- Utafiti wa Dokta Mustwafa Swaaleh Jafari kutoka Iraq usemao: (Athari za fatwa za sasa katika kusahihisha uwelewa mbaya wa hadithi ya Mtume isemayo: (Atakapo hukumu kiongozi kwa juhudi yake akapatia ana malipo mawili, na atakapo hukumu kwa juhudi yake akakosea ana malipo moja) kama mfano).

Kikao hiki kilipambwa na uchangiaji wa maoni na maswali kuoka kwa wahudhuriaji, ambao walionekana kua na hamasa kutokana na maelezo ya tafiti hizo, watafiti walisherehesha tafiti zao na wakajibu maswali.

Mwisho wa kikao hicho watafiti walipewa zawadi.

Kumbuka kua mada za kitafiti ni sehemu muhimu ya kongamano hili, na zilikua kama zifuatavyo:

  • 1- Athari ya misingi ya Ashura katika kuendelea kukubalika kwa fatwa tukufu ya kujilinda.
  • 2- Khutuba za kidini baina ya msimamo mkali na wa kawaida / khutuba za jihadi za kisasa kama mfano.
  • 3- Sehemu na athari yake katika kutangaza kulinda maeneo matakatifu / baina ya Karbala ya jana na ya sasa.
  • 4- Mtazamo wa vyombo vya habari vya Kimagharibi kuhufu fatwa ya kujilinda na athari yake.
  • 5- Athari ya fatwa katika kupambana na fitna ya ubaguzi na kujenga umoja wa kitaifa.
  • 6- Mchango wa mwanamke mwenye malezi ya Ashura katika kulinda maeneo matukufu.
  • 7- Athari ya vyombo vya habari katika kufanikisha ushindi.
  • 8- Athari za misingi ya kiimani katika kujemga moyo wa jihadi / Buriri bun Khadhiri (a.s) kama mfano.
  • 9- Athari ya malezi mema katika kumjenga mtu / Ummul Banina (a.s) kama mfano.
  • 10- Haki za binadamu baina ya uwelewa wa Ashura na Marjaiyya dini na umoja wa mataifa.
  • 11- Sifa za kiongozi na uongozi baina ya ushindi na kushindwa kwa kulinganisha matukio ya Ashura na Hashdi, uongozi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) kama mfano.
  • 12- Athari ya dua katika kujenga moyo wa mujahidina (mpiganaji) / dua ya Thughuur katika kitabu cha Swahifatu Ssajjaadiyya kama mfano.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: