Hafla ya usomaji wa Qur’an ndani ya haram tukufu ya Abbasi yahitimisha ratiba ya siku ya tatu ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada awamu ya kumi na nne…

Maoni katika picha
Siku ya tatu ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada awamu ya kumi na nne, jioni ya Juma Pili mwezi tano Shabani (1439h) sawa na (22 Aprili 2018m), kimefanyika kikao cha usomaji wa Qur’an pembezoni mwa kongamano hilo, na kuhudhuriwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqar pamoja na jopo la viongozi wa Ataba na kundi kubwa la wageni wa kongamano.

Kikao hicho kilifunguliwa kwa Qur’an iliyo somwa na msomaji mahiri bwana Ali Muhammad Najmu kutoka katika mradi wa kiongozi wa wasomaji, unao simamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, aliburudisha masikio ya wahudhuriaji kwa kuwasomea aya tukufu za Qur’an, kisha akafuata Muhammad Ali Farughi kutoka Afghanistani ambaye pia alimvutia kila mtu, kisha akafuata bwana Ahmadi Jamali kutoka Iraq, na mwisho akafuata Sayyid Muhammad Jawaad Husseini kutoka Iran, wote kwa ujumla waliwavutia sana wasikilizaji kutokana na uzuri wa sauti zao na mahadhi ya usomaji wao.

Kikao hicho kikapambwa na ujumbe wa Ustadh Abbasi Suleimi kutoka Iran, ambaye alizishukuru Ataba mbili tukufu kutokana na mchango wao mkubwa katika kusaidia miradi ya Qur’an (kuhifadhi na kusoma) na namna zinavyo tilia umuhimu swala la kufanya vikao vya usomaji wa Qur’an, mwisho washiriki wakapewa zawadi.

Kumbuka kua kikao hiki ni mwendelezo wa vikao vya aina hii ambavyo hufanywa kila mwaka pembezoni mwa kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada, na hushiriki wasomaji wa kimataifa kutoka nje na ndani ya Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: