Kwa ajili ya kuonyesha historia zake kimasomo: Shule za Ameed zashiriki katika kongamano la mwaka la (shule yetu nyumba yutu)…

Maoni katika picha
Shule za Ameed zilizo chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu, zimeshiriki katika kongamano la mwaka liitwalo (shule yetu nyumba yetu) linalo fanywa chini ya ofisi ya mkoa wa Karbala na yenye ushiriki mkubwa wa shule binafsi na za serikali, kongamano hili linalenga kuimarisha uhusiano wa vituo vya malezi na elimu katika mkoa wa Karbala, pamoja na mikoa mingine ya Iraq.

Mjumbe anaye shiriki katika maonyesho hayo Dokta Jalil Jaasim Hanun amesema kua, ushiriki wa kitengo cha malezi na elimu ya juu ni kwa ajili ya kuonyesha hatua za maendeleo katika mtiririko wa kihistoria wa uandishi wa vitabu vya masomo tangu kuanzishwa kwa shule za Ameed hadi leo, kongamano la (shule yetu nyumba yetu) linaelezea hatua hizo; tumeonyesha vitabu vingi vinavyo kubalika kitaifa na kimataifa, ikiwemo program ya (I maths) inayo fatwa na shirika la kizazi kijacho, na mfano wa program ya (glorious) pamoja na program zingine ambazo zimepata mwitikio mkubwa katika kongamano hili na zimesifiwa sana.

Kwa upande wake mjumbe wa kamati ya malezi katika kitengo cha malezi na elimu ya juu Ustadh Wasimu Naafi: Lengo la kushiriki katika maonyesho haya ni kutaka kuonyesha kinacho patikana katika shule za Ameed ambacho ni tofauti na taasisi zingine, kwa hiyo kuna program mbalimbali zilizo toa mafanikio makubwa zinazo onyeshwa hapa, kama vile; (program ya Mahdi, sikio sikivu, faqihi mdogo, makuzi ya roho, misingi ya akhlaq na zinginezo), pamoja na selebasi na vitabu vya malezi kama vile: (selebasi ya mfano wa mwezi wa michezo ya watoto, selebasi ya tunajifundisha ili tuhuishe elimu za wakubwa, mwongozo wa malezi ya kimaadili na vinginevyo).

Mjumbe mwingine wa kamati inayo shiriki katika kongamano hili Ustadh Aadil Karkushi amesema kua: Kutokana na mwaliko tulio pata kutoka katika ofisi ya malezi ya mkoa wa Karbala, tumekuja kushiriki katika kongamano la (shule yetu nyumba yetu) linalo fanyika katika shule ya Haidariyya ya wasichana, chini ya usimamizi wa ofisi ya malezi ya mkoa wa Karbala, ofisi hiyo imefanya kila iwezalo ili kuwarahisishia washiriki, kama vile kuandaa maeneo maalumu yanayo tumiwa na washiriki, jambo ambalo limetupa fursa ya kuonyesha ratiba za masomo zilizo kua tukitumika miaka ya nyuma pamoja na zinazo tumika mwaka huu, tunafurahi sana kupata fursa ya kushiriki katika kongamano hili kwani tumepata mwitikio mkubwa na watu wameonyesha kufurahishwa na sisi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: