Maonyesho ya vitabu ya kimataifa ya Karbala yashuhudia hafla ya kusaini kitabu cha (Mazuri ya majaalisi za Karbala)…

Maoni katika picha
Maonyesho ya vitabu ya kimataifa ya Karbala, hayakuishia kuonyesha vitabu peke yake, kulikua na shughuli zingine za ziada, kama vile hafla ya kutia saini kitabu, jambo hilo ni miongoni mwa mambo muhimu katika maonyesho ya kimataifa, asubuhi ya Juma Tatu (6 Shabani 1439h) sawa na (23 Aprili 2018m) imefanyika hafla ya kutia saini kitabu cha (Mazuri ya majaalisi za Karbala), kilicho tolewa na kituo cha turathi za Karbala / kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kilicho andikwa na Ustadh Salmaan Haadi Aali-Twa’ma.

Ustadh Salmaan Aali-Twa’ma alizaliwa Karbala mwaka wa (1935m) katika familia tukufu ya Ma-Alawiyya, wanajulikana kama Masayyid wa Aali-Twa’ma ambao ni tawi la kabila la Aali Faaiz Ma-Alawiyya ambayo ni kabila ya mwanzo kuishi katika ardhi tukufu ya Karbala, naye alikua mshairi, mtaalamu wa lugha na mwana historia, ameandika zaidi ya vitabu (70) na kitabu chake cha mwisho ndio hiki kilicho kua kikisainiwa leo.

Muongozaji wa hafla alieleza kwa ufupi kua: “Hakika kitabu hiki (Mazuri ya majaalisi za Karbala) nimeyashuhudia mazuri hayo katika majaalisi za Karbala, sawa sawa ilikua ni katika vielelezo tegemezi au vilivyo sahaulika, vielelezo vilivyo andikwa ni vichache lakini kukutana na wahusika ndio kunako nisaidia, asilimia kubwa ya majlisi hizo nimehudhuria mimi binafsi kuanzia miaka ya hamsini hadi sasa, kama vile majlisi za Masayyid wa Aali Thaabit, na Aali Naqiib na majlisi ya Sayyid Dhiyaau-Dini mtumishi wa raudhat Abbasiyya tukufu, na majlisi ya Twamamigha na Salalima, na majlisi ya Aali Hadidi, nilikua nahudhuria asubuhi na jioni katika miaka ya hamsini karne iliyo pita”.

Akaongeza kusema kua: “Majlisi hizo zilikua zikiendeshwa na washairi, akiwemo Muhsin Abu Hubbu ambaye nilimuona na nilihudhuria majlisi zake, alifariki mwaka wa (1949m), pamoja na washairi wengine kama vile Aali Huru na Aali Kubba na wengineo, nilikua naona wakibadilisha mawazo baina yao kuhusu yanayo tokea katika majlisi zao, kulikua na majaalisi za shule za dini, mfano shule ya Badakuba, Ruqaa, Hassan khan na shule ya Hindiyya kubra na Hindiyya sughra pamoja na shule ya Allamah bun Fahdi Hilliy, na zinginezo ambazo tulikua tunahudhuria majlisi zake pamoja na washairi hao, nilihudhuria majlisi nyingi ambazo zinaweza kufuka (80) takriban, na nilijifungisha mambo mengi kutokana na wao”.

Rais wa kamati ya maonyesho Dokta Mushtaqu Ali amesema ku: “Hakika hafla ya kutia saini kitabu ni jambo linalo fanywa sana katika maonyesho ya kimataifa, lengo ni kumtambulisha zaairu na vituo vingine vya usambazaji toleo la mwisho la mtunzi wa kitabu kinacho sainiwa na kutoa historia kwa ufupi kuhusu muandishi na vitabu vyake, ili isaidie kujenga soko la kitabu hicho”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: