Pembezoni mwa kongamano la wanawake la nane ambalo limefanywa sambamba na kongamano la Rabiu Shahada awamu ya kumi na nne, na kufuatia kemeo la Marjaa dini mkuu lililo tolewa katika khutuba ya Ijumaa kuhusu ongezeko la talaka na mpasuko wa familia.
Kutokana na umuhimu wa jambo hilo, kamati inayo simamia kongamano imefanya warsha maalumu kuhusu familia, iliyo kua na mada kuu mbili, mada ya kwanza inahusu talaka, sababu zake na namna ya kujiepusha nazo.. na mada ya pili inahusu, mpasuko wa familia, sababu zake na namna ya kuziepuka.
Mada ya kwanza ilisimamiwa na Dokta Rifaa Hakim, alitoa kazi ya vikundi, na vilikua vikundi vitano, kila kikundi kilikua na watu wanne hadi watano, wajijadili kuhusu sababu za talaka na namna ya kuziepuka.
Mada ya pili pia ilijadiliwa katika vikundi vitano kila kikundi kilikua na watu wanne hadi watano, na iliongozwa na Dokta Nawaal Almayali, walijadili kuhusu matatuzo makubwa yanayo zikumba familia na kupelekea mpasuka ndani ya familia za kiislamu.
Walijikita katika hoja za kisheria, kidini na kimaumbile, kutokana na kuwepo washiriki walio bobea katika fani hizo, ili suluhisho likidhi kila sekta na waje na jibu muafaka linalo tokana na sekta zote.
Tunapenda kukumbusha kua warsha hii ilikua na washiriki (50) wasomi wa dini na sekula kutoka ndani na nje ya Iraq.