Idara inayo simamia maonyesho ya vitabu ya kimataifa yanayo fanyika Karbala ambayo ni sehemu ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada awamu ya kumi na nne, imefanya hafla ya kutoa zawadi kwa vituo vilivyo fanya vizuri katika maonyesho hayo kutokana na vigezo walivyo weka.
Hafla hiyo imefanyika jioni ya Juma Nne (7 Shabani 1439h) sawa na (24 Shabadi 2018m) katika ukumbi wa Imamu Hassan ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, na ilihudhuriwa na katibu mkuu Muhandisi Muhammad Ashiqar pamoja na jopo la viongozi wa idara zake na ujumbe unao wakilisha Atabatu Husseiniyya tukufu.
Hafla hiyo ilikua na vipengele vingi, miongoni mwa vipengele hivyo ni usomaji wa Qur’an tukufu na usomaji wa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, uwasilishaji wa ujumbe wa idara inayo simamia maonyesho ulifanywa na mkuu wa idara hiyo Dokta Mushtaqu Ali.
Halafu ukafuata ujumbe wa vituo vilivyo pewa zawadi, ulio wasilishwa kwa niaba yao na Ustadh Amaad Aaidi kutoka Lebanon. Baada yake ukafuata ujumbe wa umoja wa wasambazaji wa vitabu wa Iraq ulio wasilishwa na Ustadh Mahdi Haadi Sha’alani.
Na mwisho kabisa zikatolewa zawadi kwa vituo vilivyo fanya vizuri katika maonyesho, kwa kuanza kuwazawadia wawakilishi kutoka katika vikosi vya Hashdi Sha’abi ambavyo ni kikosi cha Ali Akbaru na kikosi cha Abbasi, kisha kikazawadiwa kituo cha habari cha Karbala na kituo cha Alkafeel cha upigaji picha na utengenezaji wa vipindi, kutokana na kuthamini mchango wao wa kutangaza maonyesho haya.