Dokta Jirisi Hayoor mwakilishi wa ujumbe wa Uingereza katika kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada awamu ya kumi na nne amesema kua: “Nina furaha kubwa kua mgeni wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kongamano la Rabiu Shahada, kuwepo kwao pamoja na sisi wakati wote, malalo yao matukufu yamejengwa vizuri sana, ni matokeo ya kazi nzuri iliyo fanywa na watumishi wa malalo hayo pamoja na wahisani, na kwa aina hiyo hiyo watu hawa wameratibu na kufanya kongamano hili kwa ustadi mkubwa sana na kila kitu kimepangiliwa vizuri”.
Aliyasema hayo katika ujumbe wake alio toa kwenye hafla ya ufungaji siku ya Juma Nne (7 Shabani 1439h) sawa na (24 Aprili 2018m).
Akaongeza kusema kua: “Inanijia fikra kua Imamu Hussein (a.s) alikua hahusiani na shia peke yao au waislamu peke yao bali ni kielelezo muhimu wa Mwenyezi Mungu kwa wanadamu wote, kongamano hili limekusanya watu wa aina zote, Shia, Sunni na Wakristo kutoka nchi tofauti na watu wanao ongea lugha tofauti, hii ni alama kubwa ya umoja wa wanadamu, sote ni watoto wa Adamu tunatakiwa kufanya mambo mema na ibada pamoja na kumpenda Mwenyezi Mungu mmoja wa pekee.
Mimi nilipo kuja hapa, hamu yangu kubwa ilikua ni kuangalia namna gani tunaweza kutekeleza wajibu wa kutambuana kwa mujibu wa mwongozo wa Imamu Hussein (a.s) na utukufu wake na tabia zake, ikiwa kweli tunakubali kua Imamu Hussein ndiye mfano mwema kwa wanadamu wote, lazima tutafute njia ya kukitambulisha kisa chake ili tuweze kuiga maisha yake, na ikiwa tunaamini dini ya asili ambayo kila mwanadamu kazaliwa katika dini hiyo, ujumbe huo unatakiwa uwafikie watu kwa namna ambayo utagusa roho ya kila atakaye usikia.
Hakika hii ni kazi tukufu sana inawafaa wapenzi wa Hussein wa hapa Karbala, hakika swala la kua na kigezo chema, na kupatikana kwa njia bora ya kukielezea kisha kuwafikia watu wote duniani kunahitaji kuwepo kwa kundi la watu wenye kufanya kazi kwa Ikhlasi, ni ipi njia nzuri ya kuhitimisha kongamano hili itakayo tuwezesha kupata baraka za Imamu Hussein na mtukufu Abbasi (a.s) katika kazi hii”.