Uongozi wa Ataba mbili tukufu wafunga pazia la kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada awamu ya kumi na nne…

Hafla ya ufungaji
Baada ya siku tano zilizo jaa ratiba za vikao vya kitafiti, usomaji wa Qur’an, mashairi, ziara na kutembelea maeneo mbalimbali, Alasiri ya leo Juma Nne (7 Shabani 1439h) sawa na (24 Aprili 2018m) imefanyika hafla ya kufunga kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada awamu ya kumi na nne lililo simamiwa na uongozi mkuu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, chini ya kauli mbiu isemayo: (kwa utukufu wa Imamu Hussein (a.s) tumepigana na kwa utukufu wa fatwa tumeshinda), kuanzia tarehe (3 Shabani) hadi (7 Shabani).

Hafla ya ufungaji ilifanyika ndani ya ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s), ilifunguliwa kwa Qur’an iliyo somwa na msomaji wa Atabatu Husseiniyya tukufu bwana Osama Karbalai, kisha ukafuata ujumbe wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, ulio wasilishwa na kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi.

Kisha ukafuata ujumbe wa Ataba za Iraq ulio wasilishwa na mkuu wa idara ya Atabatu Askariyya Mheshimiwa Shekh Sataar Murshidi.

Na Daaru Iftaa ya Iraq pia ikatoa neno lililo wasilishwa na msemaji wake rasmi Mheshimiwa Shekh Aamir Bayati.

Hafla ilipambwa na mashairi yaliyo somwa na mshairi wa kilebanoni bwana Ali Asili Aamili, beti zake zilielezea kumpenda Imamu Hussein (a.s), hali kadhalika katika hafla hii yalitangazwa matokeo ya shindano la mashairi kuhusu Imamu Hussein (a.s), kisha ukaingia wakati wa wageni wa kongamano kuwasilisha matamko yao. Ugeni wa Urusi uliwasilisha tamko lao kupitia mwakilishi wa Daaru Iftaa ya Jamuhuri ya muungano ya Urusi Mheshimiwa Shekh Haamu Bibasuun.

Baada yake ugeni kutoka Ungereza nao ukatoa tamka lao, lililo wasiliswa na Dokta Jerisi Hayoor.

Halafu likafuata tamko kutoka katika ugeni wa Marekani, lililo wasilishwa na Dokta Josefu Kolank.

Baada ya hapo masikio yakaburidishwa kwa kusikiliza mashairi murua kutoka kwa msifuji wa Hussein bwana Akili.

Hafla ikafungwa kwa kutoa zawadi kwa washiriki mbalimbali wa kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada ambao ni watafiti, watangazaji, washairi na wengineo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: