Abulfadhil Abbasi (a.s) ni mlango wa Abu Abdillahi Hussein (a.s)…

Maoni katika picha
Abulfadhil wewe ni mlango wa mjukuu wa Mtume kama alivyo kua *** Baba yako Ali mlango wa Ahmada.

Zimeandikwa kwenye mlango wa fedha katika eneo lililo pambwa kwa dhahabu ndani ya raudha ya Abulfadhil Abbasi (a.s) beti za kaswida ya khatibu mashuhuri Shekh Muhammad Ali Yaqubi, zikiwemo beti zifuatazo:

Yeye ni Mlango wa Hussein hatapata hasara hata siku moja atakaye kuja akitegemea utetezi wake.

Hakika yeye ni Mlango wa Hutwa ataogopa kila mwenye kushikamana nao.

Simama kwake uombe na ukitawasal kupitia yeye utakubaliwa dua yako.

wewe ni mlango wa mjukuu:

katika ubeti wa kwanza wa kaswida hii, mshairi anaashiria kua hakika Abulfadhil Abbasi (a.s) alifuata nyayo za baba yake Kiongozi wa waumini ali (a.s) katika imani yake na tabia zake, kutokana na ukubwa wa imani aliyo kua nayo Imamu Ali (a.s) pamoja na ubora wa tabia zake, Mtume (s.a.w.w) alikua akimtanguliza katika kila jambo muhimu, na akimwita katika kila jambo baya na zuri.

Na yeye (a.s) alikua ameiweka nafsi yake tayali kwa kumtumikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) na kumlinda, kuna neno lake mashuhuri lisemalo: (mimi ni miongoni mwa watumwa wa Muhammad s.a.w.w). Mwenyezi Mungu mtukufu alimsifu siku aliyo lala katika kitanda cha Mtume (s.a.w.w) kwa ajili ya kumlinda kwa kutumia nafsi yake, kwa kusema: (Na katika watu yupo ambaye huiuza nafsi yake kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu ni mpole kwa waja wake).

Na sehemu zingine nyingi alizo onyesha misimamo, mbaka Mtume akasema: (Mimi ni mji wa elimu na Ali ni mlango wake, atakaye taka kuja katika mji huu apitie mlangoni), hivyo Imamu Ali (a.s) alikua ndio mlango wa Mtume (s.a.w.w), alikua ndio mtu wake wa karibu zaidi awapo nyumbani au safarini, katika amani au vitani, alikua mlinzi wake kwa nafsi yake na roho yake, na mali zake na watoto wake, jambo hilo lilijulikana kwa watu hadi ikawa mtu anaye taka ukaribu na Mtume anajikurubisha kwa Ali (a.s), na anaye taka kumuona Mtume anapitia kwa Imamu Ali (a.s), na anaye taka kukidhiwa haja zake na Mwenyezi Mungu baada ya kutawasal kwa Mtume (s.a.w.w) anatawasal na Ali (a.s). hivyo ndio alivyo kua Abulfadhil Abbasi (a.s) mtoto wa Imamu Ali (a.s) kwa ndugu yake Imamu Hussein (a.s), kutokana na ukubwa wa imani yake na uzuri wa tabia, Imamu Hussein (a.s) alimtanguliza katika kila jambo, alimwita katika zuri na baya.

Na yeye (a.s) alikua amejitolea kumtumikia ndugu yake Imamu Hussein (a.s) na kumlinda hadi akajulikana kwa umaarufu wa kauli aliyo kua akiitumia kumwita ndugu yake isemayo: Bwana wangu na kiongozi wangu (Sayyidiy wa Maulaya).

Haikuwahi kujulikana hata siku moja kua alimwita kwa kusema ewe ndugu yangu, ispokua wakati mmoja tu tema mara moja katika siku ya Ashura, pindi alipo anguka kutoka katika farasi wake kutokana na uchungu wa majeraha aliyo kua nayo, ulikua muda mgumu sana, muda ambao mwanadamu hutamani kuwaona watu wake wa karibu wenye kumhami, kwani hutaka kuwatazama jicho la mwisho, ili aweze kuwaaga kwa mara ya mwisho.

Katika muda huo, na katika wakati mgumu alio kua nao Abulfadhil Abbasi (a.s) aliiruhusu nafsi yake imwite ndugu yake kwa kusema: Ewe kaka njoo umwangalie ndugu yako!.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: