Atabatu Abbasiyya tukufu yajiandaa kulinda amani na kutoa huduma bora kwa mazuwaru wa nusu ya mwezi wa Shabani…

Maoni katika picha
Vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu vinajiandaa kulinda amani na kutoa huduma kwa wageni wanao kuja kufanya ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani ambayo itakua usiku wa Juma Tano (2 Mei 2018m) sawa na (15 Shabani 1439h), kwa kiwango ambacho watatoa ulinzi mkubwa na huduma bora. Kila kitengo kinacho husika na kutoa huduma za moja kwa moja kwa mazuwaru kimeanza kujiandaa kutoa huduma bora kulingana na aina ya huduma zao, na wanasubiri ruhusa ya kuanza kutekeleza ratiba zao kutoka kwa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa mujibu wa taarifa tulizo pata, hakika vitengo vyote vimejipanga kuimarisha ulinzi na kutoa huduma bora huku wakitumia uzowefu wa siku za nyuma walio nao, kila kiongozi wa idara ameandaa ratiba ya utendaji wa idara yake na kuiwasilisha kwa viongozi wakuu kisha ikajadiliwa kwa pamoja kwa kuangalia usalama wake na huduma zake, kwani lengo ni kutoa huduma bora kabisa na kuweka mazingira ya amani na utulivu utakao wawezesha mazuwaru kufanya ibada kwa utulivu na urahisi, na idara zote zinafanya kila ziwezalo kwa ajili ya kufikia lengo hilo.

Kumbuka kua ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani ambayo inafungamana na kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Mahdi (a.f) ni ziara ya pili kwa kua na watu wengi (mamilioni ya watu) ambao huja katika Ataba tukufu za Karbala baada ya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) ambayo hufanywa tarehe ishirini ya mwezi wa Safar.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: