Kwa maboresho ya kiufundi: Mtandao wa kimataifa Alkafeel unamwenekano mpya na wakupendeza…

Maoni katika picha
Kutokana na maendeleo ya sasa hususan ya simu za kisasa (smart phone) na ili kufanikisha kuzitumia kwa njia sahihi, watalamu wa idara ya Intanet chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu wanaendelea kutengeneza aprication mpya za kisasa za mtandao wa kimataifa Alkafeel zinazo tumika katika simu za kisasa za (smart phone), aprication ambazo ni rahisi kuzitumia tofauti na zile za zamani.

Kwa mujibu wa maelezo ya wasimamizi wa jambo hili, wamesema kua aprication hizo zinasifa zifuatazo:

  • 1- Zimetengenezwa vizuri na zinavutia.
  • 2- Zimeongezwa kipengele cha matangazo mubashara kilichopo katika mtandao rasmi.
  • 3- Kuna mabadiliko katika kipengele cha maktaba ya picha kimeongezewa sehemu ya (pendeza, pakua na shiriki).
  • 4- Kuna mabadiliko katika kipengele cha picha za video, kimewekewa njia rahisi ya kufungua na kuangalia video.
  • 5- Mpangilio mpya wa ziara kwa niaba unao muwezesha mtumiaji kufungua Acount maalumu anayo weza kuitumia kwa kujisajili kwa ajili ya ziara.
  • 6- Mpangilio mpya wa rekodi za sauti unao muwezesha msikilizaji kuperuzi kwa urahisi.
  • 7- Kurahisisha utokezaji wa alama, zinatokeza haraka na kwa muonekano mzuri tofauti na zamani.
  • 8- Kimeongezwa kipengele cha “tafuta” ndani ya picha.
  • 9- Kuboresha na kuharakisha ufungukaji wa vipengele.
  • 10- Uwezekano wa kufunguka kwa kiwango kinacho endana na uwezo wa Intanet.

Kumbuka kua mtandao wa kimataifa Alkafeel ndio mtandao rasmi wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika simu za kisasa (smart phone) unajumuisha milango na kurasa nyingi, kama vile, habari za Ataba tukufu, maktaba ya sauti, maktaba ya picha na ziara kwa niaba, aprication hii imetengenezwa na watalamu wa idara ya Intanet chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: