Atabatu Abbasiyya tukufu yasimamia hafla ya kukhitimisha harakati za Qur’an za Madrasat Fadak Zaharaa...

Maoni katika picha
Chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, Madrasat Fadak Zaharaa (a.s) imekhitimisha harakati yake ya usomaji wa Qur’an ya mwaka wa tano, katika ukumbi wa jengo la Imamu Haadi (a.s) lililo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu iliyo somwa na Muslim Aqiil, kisha ukafuata ujumbe wa kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi, ulio wasilishwa kwa niaba yake na mjumbe wa kamati kuu ya uongozi Sayyid Adnaan Mussawi, alianza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mtukufu, na akasifu kufanyika kwa harakati za aina hii zinazo saidia kujenga jamii njema chini ya misingi ya kiislamu, akawasifu watendaji kutokana na juhudi kubwa waliyo fanya kwa ajili ya kufanikisha mradi huu wenye faida za kidini na kijamii.

Akasisitiza kua: “Hakika fatwa tukufu ya jihadi ya kifaya, na damu takatifu ya mashahidi iliyo mwagika kwa ajili ya kuilinda Iraq na raia wake pamoja na maeneo matukufu ina athari nyingi, zikiwemo athari za kijamii ambazo mmezielezea kupitia picha tunazo ziona katika hafla hii tukufu”.

Ukafutia wakati wa kukabidhi cheti kwa hafidhi na msomaji wa Qur’an tukufu Zainabu Hussein, kisha zikafuata nasaha zilizo sisitiza umuhimu wa Qur’an katika maisha ya wanadamu hapa duniani na akhera, miongoni mwa yaliyo semwa ni: “Hakika Qur’an tukufu ina athari kubwa sana katika kunufaika na wakati, kila mwanafunzi wa madrasa au chuo kikuu asome na kuhifadhi Qur’an tukufu, na afuate mafundisho ya Qur’an katika maisha yake, mwanafunzi wa shule akishikamana na Qur’an atakua mfano kwa senzake, vivyo hivyo mwanafunzi wa chuo hali kadhalika mama wa nyumbani, na hao ndio walezi wakuu wa jamii, wanao weza kuwafundisha watoto maadili mema na kutengeneza jamii inayo fuata mafundisho ya Qur’an tukufu.

Ukafuata ujumbe wa mkuu wa Madrasat Fadak Zaharaa (a.s) Mheshimiwa Ummu Abdillahi, miongoni mwa aliyo sema ni: “Kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu ametoa ushirikiano mkubwa katika Madrasat Fadak Zaharaa (a.s) kwa ajili ya kuakikisha Madrasa hii inaendelea na kutoa fursa kubwa ya usomaji wa Qur’an kwa wanawake”.

Akafafanua kua: “Juhudi ninazo fanywa na Madrasa hii ya Qur’an zinatokana na taufiki ya Mwenyezi Mungu mtukufu, lengo letu kubwa ni kumridhisha Mwenyezi Mungu mtukufu na Ahlulbait (a.s). Madrasa hii inafanya kazi kama kundi la nyuki, kwa kushirikiana baina ya wanafunzi na walimu, ushirikiano huo unanafasi kubwa ya kua na idadi kubwa ya wanafunzi walio hifadhi Qur’an tukufu”.

Hafla ilikua na vipengele vingi, kikiwemo kipengele cha maswali kuhusu hukumu za tajwidi, ambayo yalivutia sana wahudhuriaji, pia kulikua na kipengele cha kusoma sehemu ya khutuba ya Imamu Ali (a.s) aliyo waelezea wacha Mungu, ilisomwa na mwanafunzi aitwaye Nuru Zaharaa Walidi, mwisho wanafunzi waliimba kaswida kuhusu Qur’an tukufu.

Hizi ni shughuli muhimu katika jamii kwani zina mchango mkubwa wa kurekebisha nafsi, na kutengeneza jamii yenye maadili mema inayo fuata sheria za Mwenyezi Mungu kama zilivyo fundishwa na Mtume (s.a.w.w).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: