Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chatangaza kukamilika kwa maandalizi ya mawakibu za kutoa huduma zitakazo shiriki katika ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani…

Bwana Riyaadh Ni’mat Salmaan.
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu za Husseiniyya za hapa Iraq na katika ulimengu wa kiislamu kilicho chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimetangaza kukamilika kwa maandalizi yote ya kiusalama na kiutumishi kwa ajili ya mawakibu za Husseiniyya zitakazo shiriki katika ziara ya Shaabaniyya itakayo fanyika siku ya Juma Tano ijayo (15 Shabani 1439h) sawa na (2 Mei 2018m).

Rais wa kitengo hicho bwana Riyaadh Ni’mat Salmaan ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kua: “Hakika ziara ya nusu mwezi wa Shabani ni ziara ya pili kwa kuhudhuriwa na watu wengi hapa Karbala na katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, imekua kawaida kwa watu wenye maukibu wa ndani na nje ya Mkoa wa Karbala kushiriki katika kutoa huduma ya chakula, vinywaji na vitu vingine kwa mazuwaru hao”.

Akaongeza kusema kua: “Baada ya kitengo chetu kutangaza maukibu zinazo penda kutoa huduma zije kujiandikisha katika ofisi yetu moja kwa moja au kwa kutumia wawakilishi wetu waliopo mikoani, tayali zimesha jitokeza maukibu nyingi na tumesha ainisha sehemu ya kila maukibu pamoja na kuvitaarifu vyombo vya usalama vya mji wa Karbala, hali kadhalika tumesha kamilisha taratibu za kiidara ikiwa ni pamoja na kuandaa vitambulisho maalumu kwa kila maukibu”.

Akafafanua kua: “Tumesha toa maelekezo kwa vikundi vya maukibu kuhusu utekelezaji wa kazi zao katika kipindi chote watakacho kuwepo hapa Karbala, kwa ajili ya kulinda heshima ya mji huu mtukufu na kuhakikisha mazuwaru wanafanya ibada kwa amani na utulivu”.

Akasisitiza kua: “Kuna mawakibu tayali zimesha anza kufanya kazi ya kutoa huduma na zingine zinaandaa maeneo yao ndani na nje ya mji wa karbala na katika njia zinazo elekea Karbala”.

Kumbuka kua ziara ya nusu mwezi wa Shabani ambayo inafungamana na kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Mahdi (a.f) ni ziara ya pili yenye kuhudhuriwa na watu wengi katika Ataba tukufu za Karbala baada ya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) ambayo hufanyika tarehe isharini mwezi wa Safar, Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimejipanga kuimarisha usalama na kutoa huduma kwa kiwango kinacho endana na wingi wa watu watakao kuja kufanya ziara.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: