Raudhatu Ahbaabul Kafeel ya Qur’an yafanya mahafali ya kumaliza awamu ya tano ya wanafunzi wake…

Sehemu ya mahafali
Raudhatul Kafeel ya Qur’an katika Maahadi ya Qur’an tukufu tawi la wanawake ambalo lipo chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kauli mbiu isemayo: (Kutoka ndani ya Saaqi tunakata kiu ya Qur’an) imefanya mahafali ya kumaliza masomo kwa wanafunzi wake wa awamu ya tano wanao itwa wapenzi wa Alkafeel”.

Mahafali hiyo imefanyika katika ukumbi wa chuo kikuu cha Alkafeel kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika mkoa wa Najafu na kuhudhuriwa na wanafunzi pamoja na walimu wao, baada ya Qur’an ya ufunguzi, mkuu wa Maahadi hiyo Ustadhat Mannaar Jawaad Aljuburi alibainisha kua: “Hakika kipindi cha utoto ni kipindi muhimu sana, kinabeba nafasi kubwa ya malezi, kwa sababu anacho jifunza mtoto katika wakati wa utoto wake kitakuja kumnufaisha baadae katika maisha yake, hivyo miongoni mwa vipaombele muhimu ni kundi la watoto, kwa sababu umri huo ndio msingi muhimu katika maisha yote ya mwanadamu”.

Akamaliza kwa kusema: “Tunawashukuru sawa walimu na viongozi wa idara ya watoto kwa juhudi kubwa wanayo fanya ya kulea watoto hawa na kuwafundisha kitu chenye thamani kubwa kitakacho wanufaisha katika maisha yao”.

Mwisho wa mahafali hiyo wanafunzi wanao maliza wakapewa vyeti pamoja na watumishi wanao fanya kazi katika Maahadi hiyo.

Kumbuka kua idara ya Raudhatul Kafeel ya Qur’an ni moja ya sehemu muhimu za Maahadi ya Qur’an tukufu tawi la wanawake katika mkoa wa Najafu Ashraf, ambayo inatoa malezi mema kwa watoto yanayo endana na Qur’an tukufu kulindana na umri wao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: