Idara ya hospitali ya rufaa Alkafeel ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imekusudia kufikia kila aina ya maendelea katika sekta ya matibabu, na imepiga hutua kubwa katika hilo, majaribio yake ya kimatibabu mengi yamefanikiwa, miongoni mwa maendeleo waliyo pata ni kutumia kwao Dermasyn na Microsyn, nayo ni miongoni mwa matibabu ya kisasa zaidi kwa watu wenye sukari waliopata vidonda au majeraha au kuungua, dawa hiyo imeonyesha uwezo mkubwa wa kutibu maradhi hayo, utumiaji wa tiba ya betri hua haumalizi tatizo na aina hiyo ya matibabu tumesha achana nayo.
Haya ndio aliyo ongea mkuu wa hospitali Dokta Haidari Bahadeli kuhusu matibabu haya, alisema: “Aina hii ya miatibabu ni mpya kabisa katika maradhi haya, hospitali ya Alkafeel ni moja ya mawakala rasmi wa matibabu hayo, na tumesha pokea mamia ya wagonjwa wa sukari wenye vidonda, majeraha na hata wenye vidonda vilivyo tokana na upasuaji na wote tumefanikiwa kuwaponyesha kwa kutumia njia hii”.
Akaongeza kua: “Hospitali inamadaktari bingwa wa maradhi hayo na walio bobea katika kutumia njia hii mpya ya matibabu, tunaweza kusema hatuta tumia tena njia ya betri katika kutibu maradhi haya”.
Akamaliza kwa kusema: “Baada ya kufanikiwa kutibu makumi ya wagonjwa wa maradhi haya kwa kutumia Microsyn, tumeweza kupunguza kiwango cha sukari hadi asilimia mbili kwa mia wakati ilikua inafika hadi asilimia sitini kwa mia, hali kadhalika tumegawa bure maelfu ya vipande vya matibabu ya maradhi ya sukari ndani ya miezi minne”.
Kwa maelezo zaidi unaweza kupiga simu zifuatazo kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja Alasiri: (07717672301/ 07819434680/ 07730622240).
Unaweza kutoa oda kwa kupitia Whatsapp kwenye simu namba: (07827270312), kwa kuandika majina matatu ya mgonjwa, mkoa anao ishi na namba yake ya simu, pamoja na jina la daktari unaye mkusudia kukuwekea oda.
Kumbuka kua hospitali ya rufaa Alkafeel ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, tangu kuanzishwa kwake imesha fanya mamia ya upasuaji wa magonjwa mbalimbali na asilia kubwa ilifanikiwa, kutokana na sababu kuu mbili: uwezo wa madaktari wake wa wairaq na wageni, na ubora wa vifaa tiba walivyo navyo, ukiongeza na baraka za mwenye jina hili la Alkafeel ambaye ni Abulfadhil Abbasi (a.s).
Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zinazo tolewa na hospitali hii unaweza kutembelea toghuti ya hospitali ifuatayo: www.kh.iq au piga simu zifuatazo: (07602329999 / 07602344444)