Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zatangaza shindano la kuandika kitabu kuhusu Imamu Hussein (a.s)…

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada linalo simamiwa na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya imetangaza masharti ya kushiriki katika shindano la kuandika kitabu kuhusu Imamu Hussein (a.s) litakalo fanyika mwakani, tangazo hilo lilitolewa katika hafla ya ufungaji wa kongamano.

Shindano litajikita katika utunzi peke yake, utunzi huo uhusu mada zifuatazo:

  • - Uhusiano wa Mtume (s.a.w.w) na Imamu Hussein (a.s) katika upande wa kifiqhi, ki-itikadi na kimalezi.
  • - Wasifu wa Imamu Hussein (a.s) kiroho, kiuongozi na ki-islahi.
  • - Athari ya Imamu Hussein (a.s) katika fikra za wanadamu kiutamaduni na kielimu.
  • - Swala la Ashura (mazuri yake na mabaya yake).
  • - Historia ya Imamu Hussein (a.s) na fikra zake.
  • - Maadhimisho ya Husseiniyya (misingi yake na adhari zake).

Kamati imepanga kua vitabu vyote vitatumwa kwenye kamati ya majaji, na vinatakiwa kua na sifa zifuatazo:

  1. Kisiwe chini ya kurasa (150).
  2. Kila ukurasa uwe na maneno (250).
  3. Karatasi ziwe za ukubwa wa (A4).
  4. Hati iwe ya saizi (14) na haamishi (pembezi ya maandishi) iwe ya saizi (16).
  5. Aina ya hati iwe ni (Simplified Arabic).
  6. Kitabu kiwe na muonekano mzuri.
  7. Kitabu kitakabidhiwa katika kamati ya majaji kwa kufuata utaratibu utakao wekwa.

Kamati imepanga zawadi kwa washindi watatu wa kwanza kama zifuatavyo:

  • Mshindi wa kwanza (15,000,000) milioni kumi na tano dinari za Iraq, na kuchapisha kitabu chake na kukitafsiri katika lugha zingine pamoja na kumpa midani ya dhahabu.
  • Mshindi wa pili (12,000,000) milioni kumi na mbili dinari za Iraq, na kuchapisha kitabu chake pamoja na kumpa midani ya fedha.
  • Mshindi wa tatu (9,000,000) milioni tisa dinari za Iraq na kuchapisha kitabu chake pamoja na kumpa midani ya barunzi.

Kamati imesema kua, vitabu vyote vitakavyo pasishwa na kamati ya machaji vitachapishwa, kamati ya majaji itakua na wajumbe saba na mmoja wao atakua ni rais wa kamati hiyo, wajumbe watatu watakua ni wasomi wa sekula, huku wengine watatu wakiwa ni wasomi wa hauza, tarehe ya mwisho ya kupokea vitabu hivyo itakua ni (17 Rabiul-Awwal 1440h) siku ya kukumbuka kuzaliwa kwa Mtume (s.a.w.w), kitabu kiambatanishwe na wasifu wa muandishi hisika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: