Kitengo cha mitambo (magari) cha Atabatu Abbasiyya tukufu chaandaa zaidi ya gari (160) kwa ajili ya kushiriki kubeba mazuwaru wa nusu ya mwezi wa Shabani…

Maoni katika picha
Kitengo cha mitambo (magari) cha Atabatu Abbasiyya tukufu chatangaza kukamilika kwa ratiba ya kubeba na kuhudumia mazuwaru, kimeandaa zaidi ya rari (160) za aina mbalimbali chini ya maelewano maalumu na wahusika wa program hii. Haya yamethibitishwa na rais wa kiengo hicho Ustadh Maitham Abdul-Amiir, alieleza kua: “Hakika ziara ya Shaabaiyya ni miongoni mwa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu kutoka ndani na nje ya Iraq, miongoni mwa matatizo makubwa ambayo huyapata mazuwaru ni usafiri, kwa hiyo kitengo chetu kimefanya kila kiwezalo kwa ajili ya kupunguza tatizo hilo kwa mazuwaru na kuhakikisha wanatekeleza ibada yao kwa urahisi.

Akaongeza kusema kua: “Ratiba iliyo andaliwa na kitengo hiki baada ya kuainisha vituo vya ndani na nje vitakavyo tumika kwa ajili ya kubeba watu pamoja na kuandaa magari na watumishi, ambao wataanza utekelezaji kwa kufuata taratibu za kiusalama na kiutumishi kwa mazuwaru, hali kadhalika tumeandaa magari ya hakiba kwa ajili ya kutumika pale yatakapo hitajika iwapo kukiwa na ongezeko zaidi la mazuwaru”.

Akabainisha kua: “Kuna gari maalumu za utoaji wa huduma zitakazo shiriki pia, kama vile gari za wagonjwa, kugawa maji, kusambaza gesi, zima moto pamoja na gari maalumu zinazo beba mafundi makenika ambao wako tayali kutengeneza gari lolote litakalo haribika wakati wa kazi”.

Akaendelea kusema kua: “Watumishi wamepangwa kufanya kazi mfululizo saa (24) asubuhi na jioni”.

Kumbuka kua ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani ambayo hufungamana na kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Hahdi (a.f), ni ziara ya pili kwa kuhudhuriwa na watu wengi katika Ataba tukufu za Karbala, baada ya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) ambayo hufanywa mwezi ishirini Safar, Ataba mbili tukufu zimejipanga kuimarisha ulinzi na kutoa huduma zinazo endana na idadi kubwa ya mazuwaru inayo tarajiwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: