Sawa na vitengo vingine vya Atabatu Abbasiyya tukufu, kitengo cha Maqaamu Imamu Mahdi (a.f) kimetangaza kua kimekamilisha maandalizi ya kupokea mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s) katika usiku wa nusu ya mwezi wa Shabani na wahuishaji wa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa muokozi wa binadamu Imamu Swahibu Zamaan (a.f), ambapo program zimeanza muda mfupi za kuandaa mazingira kwa ajili ya kufanya ibada hizi tukufu.
Makamo rais wa kitengo cha Maqaamu Ustadh Muhammad Harabi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hakika watumishi wa Maqaamu wamejipanga kuimarisha ulinzi na kutoa huduma pamoja na kufanya kila kitu kitakacho saidia kufanikisha ibada hii tukufu, maandalizi haya hufanywa kila msimu wa ziara ya Shaabaniyya unapo fika, zimepanuliwa kumbi za wanaume na wanawake sambamba na sehemu za kuweka niatu na vitu”.
Akaongeza kusema kua: “Hali kadhalika tumeandaa maji mazuri ya kunywa na sehemu tulivu za kuswalia pamoja na kutengeneza vyoo vya kutosha, pia tumeandaa mimbari nje ya Maqaamu ambayo inatumika kwa kusoma ziara maalumu ya Abu Abdillahi Hussein (a.s) katika usiku huu mtukufu pamoja na kutoa maelekezo ya dini na fadhila za ziara ya siku hii tukufu, na kuwajulisha vijana umuhimu wa kushikamana na ziara”.
Akabainisha kua: “Hakika kazi zetu ni sehemu ya kazi za vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu na huzifanya kwa kuwasiliana nao, tumeandaa wafanya kazi wa kujitolea (300) kwa ajili ya kuwasaidia watumishi wa kitengo hiki, hali kadhalika tumeandaa sehemu litakapo fanyika kongamano la kuwasha mishumaa litakalo yanyika jioni ya leo”.
Tunapenda kufahamisha kua Maqaamu ya Imamu Mahdi (a.f) ipo upande wa kushoto wa mto wa Husseiniyya wa sasa unapo ingia Karbala kwa upande wa kaskazini ukiwa unatokea upande wa mlango wa Salama, Maqaamu inaangalia upange wa barabara ya Sidra ambayo ipo mkabala na haram ya Imamu Hussein (a.s) upande wa kaskazini, na ipo umbali wa mita (650) takriban, ni mazaru mashuhuri, ina kubba kubwa, inaitwa kwa jina la Imamu Mahdi Almuntadhir (a.f), inasemekana kua Imamu Hujjah aliswali sehemu hiyo katika moja ya ziara zake kwa babu yake Imamu Hussein (a.s), pia ni Maqaamu muhimu sana katika mji wa Karbala kutokana na kunasibishwa na Imamu Mahdi (a.f), jambo hilo limesababisha kua sehemu muhimu sana katika ziara ya Shaabaniyya, ambayo ni miongoni mwa ziara maalumu katika mji wa Karbala, mamilioni ya watu hufurika katika Maqaamu hii na pembezoni mwa mto wa Husseiniyya katika usiku wa mwezi (15) Shabani.