Jirani ya Maqaamu yafanyika kumbukumbu ya mazazi matukufu: yawashwa mishumaa (1184) imbayo ni idada ya miaka ya Imamu Mahdi (a.s)…

Maoni katika picha
Kila tunapo washa mshumaa kwa ajili ya Imamu Hujjah bun Hassan (a.f), tunaongeza matumaini ya kudhihiri kwa huyu mtu atakaye jaza haki na uadilifu hapa duniani baada ya kua imejaa dhulma na ufisadi, wapenzi wake wanasherehekea kuzaliwa kwake katika kila sehemu ya dunia, zikiwemo sherehe hizi za kuwasha mishumaa ambazo zinafanywa kwa mwaka wa kumi na nane chini ya usimamizi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, na kwa kushirikiana na mtu wa kwanza kufanya jambo hili bwana Mikdadi Karim Twaiy kutoka katika wilaya ya Swawira, na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya mazuwaru wa mji mtukufu wa Karbala pamoja na jopo la watumishi na viongozi wa Ataba mbili tukufu.

Kongamano limefanywa jioni ya mwezi (13 Shabani 1439h) sawa na (30 Aprili 2018m) karibu na Maqaamu ya Imamu Mahdi (a.f), mishumaa ilikua sawa na idadi ya miaka ya Imamu wetu (1184) ilikua imewekwa kwa namna ambayo inasomeka (Mahdi ndiye mnusuru wa waumini), maneno hayo yameandikwa kitaalamu, kila mwaka hua kuna ujumbe tofauti na mwaka ulio pita.

Hafla ilianza kwa Qur’an tukufu iliyo somwa na msomaji wa Atabatu Abbasiyya bwana Mustwafa Swaraaf, halafu ukaimbwa wimbo wa taifa kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi watukufu wa Iraq, ukafuata ujumbe wa Ataba mbili tukufu ulio wasilishwa na Shekh Maitham Zaidi mjumbe wa kamati kuu ya uongozi ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ambaye alisema kua: “Kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu tumefanikiwa kuhudhuria katika sherehe hii ya kukumbuka kuzaliwa kwa muokozi wa wanadamu (a.f) ambaye anafikisha umri wa mika (1184)”.

Akaongeza kusema kua: “Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kwa miaka mingi sasa zimekua zikisimamia na kufanya kongamano hili ambalo linajulikana kwa jina la (kongamano la mishumaa) jambo hili lilianziswa na mmoja wa waumini aliye kua anaonyesha mapenzi kwa Imamu Mahdi (a.s) kwa kutumia njia ya kuwasha mishumaa ili aweze kujikumbusha zaidi umri wa Imamu na kupendezesha sherehe hii tukufu”.

Akaendelea kusema: “Wananchi wa Iraq Mwenyezi Mungu amewapa neema nyingi na utamaduni wao umejaa katika historia, sambamba na hilo hakika ardhi ya Iraq imepata utukufu kwa kuhifadhi miili ya Maimamu sita watakasifu (a.s), pamoja na kuzaliwa kwa Swahibu Zamaan (a.f), sherehe hii inawakumbusha waumini wote waishi katika mazingira ya kusubiri, kusubiri kuna mahitaji yake, ili mtu aonekane kweli anasubiri kudhihiri kwa muokozi”.

Akafafanua kua: “Hakika fikra ya muokozi ipo katika dini zote lakini kwa maelezo tofauti, sisi tunaamini kua Mahdi ni Imamu wa kumi na mbili miongoni mwa Maimamu wa Ahlulbait (a.s), ambaye atakuja kujaza dunia haki na uadilifu baada ya kujaa dhulma na ufisadi, watu wenye kufurahia zaidi kudhihiri kwake ni watu wa Iraq, kutokana na dhulma wanazo fanyiwa kwa miongo na miongo, hivyo watu wa Iraq wana shauku kubwa ya kudhihiri kwake”.

Akamaliza kwa kusema: “Mwaka huu tunasherehekea kumbukumbu hii tukiwa katika furaha ya kuwashinda magaidi wa Daesh na kukomboa ardhi yetu, ushindi ulio patikana kutokana na fatwa ya Marjaa dini mkuu katika mji wa Najafu na mwitikio mkubwa wa Wairaq kufuatia fatwa hiyo, tunatarajia waitikie tena wito wake wa kuchagua watu waadilifu watakao liongoza taifa hili, nawashukuru sana wasimamizi wa shughuli hii na nawapongeza kwa kuidumisha kila mwaka”.

Baada yake wakafuata washairi wa Ahlulbait (a.s) walio imba kaswida zinazo husiana na tukio hili, ambao ni bwana Twalibu Farati, Falahu Barudi, Muhammad Fatwimiy na mshairi Hussam Hamzawi, na mwisho kabisa alikua ni Sayyid Ahmadi Mussawi aliye soma Dua’au Faraj, baada ya hapo wakaelekea kuwasha mishumaa.

Kongamano la mishumaa lilianzishwa na mwananchi wa Iraq tangu miaka kumi na saba iliyo pita, kabla ya kumalizika kwa utawala wa kidikteta, na limeendelea kuboreshwa hadi hivi sasa linasimamiwa na Ataba mbili tukufu kila mwaka, na limeboreshwa na kua kongamano kubwa lenye vipengele vingi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: