Miongoni mwa maandalizi ya ziara ya Shaabaniyya: Kitengo cha usimamizi wa kihandisi chafanya matengenezo kwenye jengo la vyoo…

Sehemu ya kazi
Yanafanyika maandalizi ya aina mbalimbali kwa ajili ya kuwapokea mazuwaru wa nusu ya mwezi wa Shabani na vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu, miongoni mwa maandalizi hayo ni ukarabati unao fanywa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika jengo la vyoo lililopo karibu na haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ambalo hutumiwa ba idadi kubwa ya watu.

Rais wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi, Muhandisi Abbasi Mussa Ahmadi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hakika kazi ya ukarabati inayo fanywa na kitengo chetu mfululizo kwa kufuata ratiba iliyo pangwa, kwa ajili ya kujiandaa na ziara ya Shaabaniyya, mafundi wetu wanafanya ukarabati katika jengo muhimu la vyoo, ambalo hutumiwa na idadi kubwa ya watu kila siku, jambo ambalo limepelekea kuziba kwa baadhi ya njia zake, na kulazimika kitengo chetu kifanya kazi ya kuzibua na kufanya ukarabati kwa ujumla, jengo hili lina ukubwa wa (2m350) na lina idadi kubwa ya vyoo na sehemu ya kuchukua udhu”.

Akaengeza kusema kua: “Kazi hii ya ukarabati imehusisha kuondoa vigae vya ukutani na ardhini na kuzibua njia za maji taka, pamoja na kujenga upya sakafu na kuweka vigae vya ukutani upya, sambamba na kurekebisha sehemu zote zilizo kua zimeharibika katika vyoo vyote”.

Akaendelea kusema kua: “Kazi ndani ya jengo hili imedumu kwa muda wa siku (30) mfululizo, na hivi sasa vyoo vyote vinafanya kazi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: