Fadhila na ibada za usiku na mchana wa mwezi kumi na tano Shabani…

Maoni katika picha
Usiku wa mwezi kumi na tano Shabani una utukufu mkubwa sana, imepokewa kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) anasema: (Imamu Baaqir (a.s) aliulizwa kuhusu fadhila za usiku wa mwezi kumi na tano Shabani akasema (a.s): ni usiku bora zaidi baada ya usiku wa lailatul Qadri, ndani ya usiku huo Mwenyezi Mungu huwatunuku waja wake utukufu wake na huwasamehe kwa wema wake, jitahidini kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu mtukufu katika usiku huo, hakika ni usiku ambao Mwenyezi Mungu amechukua ahadi katika nafsi yake kua hatakataa maombi ya mja wake maadam hata omba jambo la maasi, hakika ni usiku ambao Mwenyezi Mungu ameufanya kua usiku wetu Ahlulbait kama alivyo ufanya usiku wa lailatul Qadri kua ni wa Mtume wetu (s.a.w.w), jitahidini kumuomba Mwenyezi Mungu mtukufu katika usiku huo…).

Miongoni mwa baraka kubwa za usiku huu, ni usiku alio zaliwa mfalme wa umma huu na Imamu wa zama, alizaliwa mwaka wa mia mbili hamsini na tano hijiriyya katika mji wa Samara.

Zimepokewa ibada nyingi katika usiku huu, miongoni mwake ni:

  • 1- Kufanya ibada za usiku: imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Atakaye fanya ibada usiku wa mwezi kumi na tano Shabani roho yake haita kufa siku ambayo roho zitakufa”.
  • 2- Kuoga: “Hakika kunapunguza dhambi”.
  • 3- Kuswali rakaa mbili: baada ya swala ya Isha.

Namna ya swala hiyo: utaiswali kama unavyo swali swalatu Subhi, katika rakaa ya kwanza baada ya surat Fat-ha usome surat Kaafiruun, na katika rakaa ya pili baada ya surat Fat-ha usome surat Tauhiid.

Dua baada ya swala hiyo: Subhana Llahi, mara “33” Alhamdu Lillahi, mara “33” Allahu Akbar, mara “34” kisha usome Dua ya “Yaa man Ilaihi Malja-al-Ibaad…” kusujudu: na useme katika sajda: Yaa Rabbi, mara (20) ya Allah, mara (7) laa haula walaa quwata illa billahi, mara (7) maa sha-a Llahu, mara (10) laa quwata illa billahi, mara (10) kisha unamswalia Mtume Muhammad na Aali zake, halafu unaomba haja zako.

  • 4- Kumzuru Imamu Hussein (a.s): kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) anasema: “Utakapo fika usiku wa mwezi kumi na tano Shabani husamehewa dhambi za kila muumini mwenye kumzuru Hussein (a.s), na huambiwa: fanyeni ibada”.
  • 5- Kusoma dua zifuatazo: Dua ya Kumail na dua ya “Allahumma bihaqi lailatana hadhihi…”.
  • 6- Kusoma dua ya kumswalia mtume iliyo pokewa na Imamu Sajjaad (a.s): “Allahumma swali alaa Muhammad wa aali Muhammad Shajarata Nubuwwah…”

Amma ibada za mchana wa mwezi kumi na tano Shabani ni:

  • 1- Kufunga: Kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) anasema: “Itakapo fika mwezi kumi na tano Shabani, utumieni usiku wake kwa kufanya ibada na mchana wake kwa kufunga”.
  • 2- Kumzuru Imamu Hussein (a.s): “Asalamu Alaika yaa Ibnu Rasuulu Llahi”.
  • 3- Kumzuru Imamu Hujjah (a.f): “Asalamu Alaika yaa Hujjata Llahi fii Ardhihi…”.
  • 4- Duaa-ul-Ahadi: “Allahumma Rabbu Nurul Adhim…”.
  • 5- Duaau ta’ajilil-faraji, ya kudhihiri Imamu wa Zama (a.f).

(Angalia kitabu cha Mafaatihul-Janaan.. Ibada ya usiku wa mwezi kumi na tano Shabani).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: