Ilikua siku kama ya leo: Ilipo tolewa fatwa na Marjaa dini mkuu katika mji wa Najafu Ashrafu ya kuilinda ardhi ya Iraq na maeneo matukufu…

Maoni katika picha
Tuwe Wairaq wa leo na sio kama tulivyo kua kabla ya (14 Shabani 1435h), umbali huo hauwezi kuonekana kwa muda au Jografia, umbali ni mkubwa kushinda mchoro wa ramani au mshale wa saa, hali ilikua inaelekea katika ulimwengu wa kupotea, ugumu wa mzinguro ulio kua umewekwa katika miji yetu hauelezeki, kushindwa kulikua wazi kwa kila Muiraq.

Lakini ulipo chomoza mwanga wa Alfajiri ya kumbukumbu ya miaka (1180) tangu kuzaliwa kwa muokozi wa umma Imamu Mahdi (a.f) siku ya mwezi (14 Shabani) mwaka wa (1435h), ulitoka wito katika mimbari ya Ijumaa ndani ya haram tukufu ya Abul Ahraar (a.s) wito wa haki dhidi ya batili, na wito wa akili ya kiislamu dhidi ya ujinga na upumbavu uliotaka kufuta heshima ya ubinadamu kwa kutumia jina la dini ya kiislamu huku wakifanya mambo ambayo yako mbali kabisa na uislamu.

Katika mimbari ya Ijumaa na katika siku kama ya leo mwakilishi wa Marjaa dini mkuu Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai alitangaza fatwa iliyo tolewa na Marjaa dini mkuu katika mji wa Najafu ya wajibu kifaya, wa kulinda ardhi ya Iraq na maeneo matukufu dhidi ya magaidi wa Daesh.

Wananchi wa Iraq wakaitikia wito huo kwa wingi, wazee kwa vijana wakajitokeza kulinda heshima yao na maeneo matukufu, wakakomboa ardhi na wakashinda mauti, hakika maisha mazuri ni kuiona Karbala karibia na usiku wa nusu ya mwenzi wa Shabani (1439h)..
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: