Watu wanamiminika kwa wingi katika Ataba za Karbala kufanya ziara tukufu ya Shaabaniyya…

Maoni katika picha
Katika mazingira tulivu na mazuri ndani ya haramu tukufu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), Ataba hizo tukufu Husseiniyya na Abbasiyya pamoja na maeneo mengine baada ya Adhuhuri ya leo zimeshuhudiwa watu wengi wakimiminika kuja kufanya ziara tukufu ya Shaabaniyya kutoka ndani ya mkoa wa Karbala na mikoa mingine ya Iraq, na mazuwaru kutoka katika nchi za kiarabu na kiajemi.

Watu walianza kumiminika baada ya swala ya Dhuhuraini na wakaendelea hadi karibu na swala ya Maghribaini chini ya ulinzi mkali na huduma bora zinazo tolewa na watumishi wa Ataba mbili tukufu pamoja na kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu.

Watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya wanafanya kila wawezalo kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa mazuwaru, inayo endana na idadi kubwa ya mazuwaru hao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: