Miongoni mwa utaratibu ulio jiwekea mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), ni kuandaa maelfu ya sahani za chakula na kukigawa kupitia sehemu mbalimbali za kugawia chakula, chakula hicho hakikulenga mazuwaru peke yao, bali kulikua na chakula cha watumishi na wafanyakazi wa kujitolea pamoja na wageni wa Ataba tukufu.
Rais wa kitengo cha mgahawa bwana Kadhim Abada ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hakika maandalizi kwa ajili ya ziara hii yalianza mapema, tulijaza stoo za mgahawa vyakula vya aina mbalimbali, pamoja na maji, juisi na vinginevyo miongoni mwa vitu tulivyo hitajika kwa ajili ya ziara ya Shaabaniyya, pindi watu walipo anza kumiminika katika mji wa Karbala kwa ajili ya kufanya ziara, watumishi wetu wakaanza kupika chakula kwa wingi na kukigawa kwa mazuwaru”.
Akaongeza kusema kua: “Hakika ugawaji wa chakula katika kipindi hiki cha ziara, hauhusishi chakula maalumu wala muda maalumu, ugawaji wa chakula unafanyika saa zote kuanzia asubuhi hadi jioni, katika sehemu tatu, ambazo ni: Mgahawa wa Atabatu Abbasiyya, Mgahawa wa watumishi pamoja na barabara ya kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ugawaji wa chakula unaendelea vizuri na kwa kasi kubwa”.
Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu ilikua imesha tangaza kukamilika kwa maandalizi yote ya kuwapokea mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) wanao kuja kufanya ziara katika usiku na mchana wa mwezi kumi na tano Shabani, walikua wamejipanga vizuri katika kuimarisha ulinzi na kutoa huduma waliyo sema kua itachangia kurahisisha utekelezaji wa ibada kwa amani na utulivu, wametumia uwezo wao wote kwa ajili ya kufanikisha swala hilo.