Kitengo cha dini chatoa mafunzo na maelekezo ya kiislamu kwa mazuwaru wa Shabaniyya…

Maoni katika picha
Miongoni mwa ratiba za kuhuisha ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani iliyo pangwa na kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu ni kutoa mafunzo ya dini katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa nyakati tofauti, na inaendelea kipindi chote cha ziara.

Mihadhara inayo tolewa imejikita katika mafunzo ya dini, pamoja na kufafanua malengo ya ziara hii na namna ya kunufaika nayo, nayo ni sehemu tu ya ratiba iliyo pangwa na kitengo hicho ambayo mashekhe wamechukua jukumu la kuitekeleza, kutokana na utukufu wa ziara hii ambayo kila mtu anajitahidi kunufaika kiasi awezavyo.

Hali kadhalika kitengo hiki kupitia watumishi wake kinajibu maswali ya mazuwaru kuhusu mambo ya Ibaadaati na muamalaati pamoja na mambo mengine mbalimbali, pia kuna kipengele cha kufundisha surat Fat-ha kwa mazuwaru, vilevile kitengo hiki kimewapanga watumishi wake ndani na nje ya haram kwa ajili ya kurekebisha hijabu na kuwasisitiza wasichana wanaokuja kufanya ziara wazingatie uvaaji sahihi wa hijabu na walinde heshima na utukufu wa eneo hili, aidha kitengo kimeweka screen nje ya Ataba tukufu zinazo onyesha mafundisho maalumu ya kidini na kimaadili kuhusu ziara hii.

Kumbuka kua lengo la ratiba hii ni kunufaika na ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani, na kuhakikisha watu wanafanya ibada sahihi zilizo fundishwa na Ahlulbait (a.s) na kuutumia vizuri msimu wa ziara.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: