Kituo cha afya cha Atabatu Abbasiyya tukufu chatoa huduma za matimabu katika ziara ya Shaabaniyya…

Maoni katika picha
Kituo cha afya cha Atabatu Abbasiyya tukufu kinatoa huduma za matibabu bure kwa mazuwaru wa Shaabaniyya kwa kushirikiana na idara ya afya ya mkoa wa Karbala.

Kipengele hiki ni sehemu ya ratiba ya kuwahudumia mazuwaru wa mwezi kumi na tano Shabani iliyo pangwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, kipengele hiki kimehusisha vitu vingi, ikiwa ni pamoja na kuandaa madaktari na wauguzi wa ziada kwa kushirikiana na idara ya afya ya mkoa wa Karbala ili waweze kutoa huduma saa (24).

Kituo hicho kina vifaa tiba vingi pamoja na daya za aina mbalimbali, hali kadhalika tumeandaa mitungi ya Oxygen na vifaa vingine vinavyo saidia katika matibabu ya huduma ya kwanza, aidha tumesambaza gari za wagonjwa za Atabatu Abbasiyya sehemu mbalimbali, zenye dawa na vifaa tiba vyote vinavyo hitajika katika mazingira ya dharura, ambazo zipo tayali wakati wote kubeba wagonjwa na kuwapeleka katika hospitali za karibu tulizo kubaliana nazo (hospitali ya Hussein au hospitali ya Safiir ambazo zipo chini ya Atabatu Husseiniyya tukufu).

Kumbuka kua kituo cha afya chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na udogo wa eneo lake, lakini kinatoa huduma kubwa za kimatibabu, na kinafanya kazi katika kipindi choto cha mwaka, lakini siku za ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu huongeza utendaji wake zaidi, kwa kiasi ambacho kinaendana na ongezeko la watu wanao kuja kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: