Kitengo cha utumishi kimeonyesha juhudi kubwa katika kuwahudumia mazuwaru wa nusu ya mwezi wa Shabani…

Maoni katika picha
Kitengo cha utumishi ni miongoni mwa vitengo vinavyo toa huduma za moja kwa moja kwa mazuwaru, wakati wa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, ikiwemo ziara ya mwezi kumi na tano Shabani, katika ziara hii kimefanya kila kiwezalo kwa ajili ya kutengeneza mazingira bora ya kufanya ibada kwa urahisi na utulivu.

Rais wa kitengo cha utumishi bwana Khalil Mahdi Hanuun ameuambia mtandao wa Alkafeel kuhusu maandalizi waliyo fanya kwa ajili ya ziara hii, kua: “Kitengo cha utumishi kilianza maandalizi mapema, kwa ajili ya ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani, kwa kushirikisha idara zake zote, pamoja na kuziongezea idadi kubwa wa wafanya kazi wa kujitolea, kitengo hiki kinafanya kazi za aina tofauti kutokana na idara husika, kuanzia kazi za nje hadi ndani ya haram tukufu, kazi hizo ni kama zifuatazo:

  • 1- Tumeandaa idadi kubwa ya gari za kuchaji kwa ajili ya kubeba mazuwaru na kuwaleta karibu na haram tukufu.
  • 2- Tumeandaa kiasi kikubwa cha maji ya kunywa na kuyasambaza katika vituo vya kugawa maji vilivyopo ndani na nje ya haram tukufu, pamoja na kusambaza maji kwa mawakibu (vikundi) vya kuhudumia mazuwaru.
  • 3- Tumeandaa kiasi kikubwa cha barafu na kuzisambaza kwenye mawakibu zinazo hudumia mazuwaru.
  • 4- Tumeandaa na kupangilia sehemu za kuvulia viatu.
  • 5- Tumeandaa na kupangilia sehemu za kuweka vitu (Amaanaat) katika mabanda na masanduku yanayo zunguka eneo la haram.
  • 6- Tumeandaa na kutandika baadhi ya maeneo ya haram kwa ajili ya kulala mazuwaru watukufu.
  • 7- Tumefanya kazi ya kuwaelekeza mazuwaru sehemu za kupita kwa kuingia na kutoka ndani ya haram kwa ajili ya kufanya ziara.
  • 8- Tumesambaza maua mazuri kutokana na kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Mahdi (a.f) ndani na nje ya haram tukufu.
  • 9- Tumesaidia kufanya usafi ndani na nje ya haram tukufu, na tumesambaza zaidi ya pipa za kutupia (300) za kutupia taka, na (tani 7) za mifuko ya kukusanyia uchafu, kwa ajili ya kuhakikisha mji unakua msafi na kurahisisha utendaji wa magari ya kukusanya taka.
  • 10- Kutokana na kuongezeka kwa kiwango cha joto, tumeweka miamvuli mingi katika njia zinazo tumiwa na mazuwaru.
  • 11- Tumesaidia utekelezaji wa swala ya jamaa, kwa kuandaa maneneo ya kuswalia na kutandika miswala.
  • 12- Tumeandaa viti vya mataili kwa ajili ya watu wenye ulemavu na kuviweka karibu na milango ya kuingia katika haram tukufu”.

Kumbuka kua ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani ambayo hufanyika sambamba na kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Mahdi (a.f), ni ziara ya pili kwa kuhudhuriwa na watu wengi baada ya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) ambayo hufanyika mwezi ishirini Safar.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: