Upande wa kushoto wa mto Husseiniyya wa sasa, unapo ingia Karbala kwa kutokea upande wa kaskazini katika eneo la Baabu Salama kuna Maqaamu ya Imamu Mahdi (a.f), upande wa kaskazini wa kaburi la Imamu Hussein (a.s) umbali wa mita (650) takriban, ni mazaru mashuhuri na ina kubba kubwa, mazaru hii imeitwa jina la Imamu Mahdi msubiriwa (a.f), inasemekana kua Imamu Mahdi aliswali katika eneo hilo alipo kuja kumzuru babu yake Imamu Hussein (a.s).
Hii ni miongoni mwa mazaru muhimu sana katika mji wa Karbala, kutokana na kufungamana kwake na Imamu Mahdi (a.f), na hua ni sehemu muhimu katika ziara ya Shaabaniyya ambayo ni miongoni mwa ziara maalumu katika mji wa Karbala.
Kama kawaida.. katika usiku na mchana wa nusu ya mwezi wa Shabani waumini huelekea katika Maqaamu ya Imamu Mahdi (a.f), ambayo ndio siku ya kuzaliwa kwake, na kitu ambacho huvutia watu wengi ni uwashaji wa mishimaa pembezoni mwa mto wa Husseiniyya sehemu ilipo Maqaamu hiyo.
Baadhi yao huweka mishumaa juu ya ubao au mfano wa ubao na huzimika kwa maji, wamezowea kuiwasha katika usiku kama huu na huweka nadhiri za kukidhiwa haja zao na Mwenyezi Mungu kwa baraka ya Imamu wa Zama (a.f), na utukufu wa siku ya kuzaliwa kwake ambayo ni siku bora zaidi ya kukubaliwa maombi ya waja.