Wanahabari wa Atabatu Abbasiyya tukufu wamefanya kazi kubwa ya kutangaza matukio ya ziara ya mwezi kumi na tano Shabani…

Chumba cha matangazo mubashara cha Atabatu Abbasiy
Kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kufanikiwa kwa utaratibu wake wa kurusha matukio ya ziara ya mwezi kumi na tano Shabani kupitia njia mbalimbali, (Luninga, Redio, majarida na mitandao ya kijamii) zaidi ya aina 50.

Kwa mujibu wa maelezo ya makamo rais wa kitengo cha habari, Sayyid Aqiil Abdulhussein Yasiri, ambaye amesema kua: “Tumefanya kila tuwezalo kuhakikisha tunatangaza matukio ya ziara hii na kuyafikisha kwa wapenzi wa Ahlulbait wa mashariki na magharibi ya dunia, kupitia masafa mbalimbali, ikiwemo masafa ya bure kwa vituo vya luninga iliyo kua ikirusha habari muda wote, pamoja na kuzingatia ubora wa picha zilizo kua zikirushwa kutoka maeneo mengine kama vile Maqaamu ya Imamu Mahdi (a.f), eneo la katikati ya haram mbili pamoja na picha zinazo toka katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, huduma hii imenufaisha zaidi ya vituo (20) vya luninga kutoka ndani na nje ya Iraq, kazi yote imefanywa na watalamu wa kituo cha uzalishaji cha Alkafeel cha matangazo ya moja kwa moja (mubashara)”.

Akaongeza kusema kua: “Hali kadhalika tuliwarahisishia wanahabari wa kitaifa na kimataifa utendaji kazi wao, waliweza kuripoti matukio kwa urahisi, pia kituo chetu kiliripoti matukio ya ziara moja kwa moja kwenye vituo vya luninga na vyombo vingine vya habari”.

Akaendelea kusema kua: “Kuhusu urushaji wa habari kwenye mitandao ya kijamii, kazi hiyo ilisimamiwa na mtandao wa kimataifa Alkafeel kupitia kamati zake zinazo husika na mitandao ya kijamii, nao walirusha matukio kutokana na taarifa za habari na picha, Redio ya Alkafeel ya mwanamke wa kiislamu ambayo ipo chini ya kitengo chetu, iliandaa vipindi maalumu kuhusu malengo ya ziara na namna ya kunufaika nayo, kuhusu upande wa habari za kusomwa, jarida la Swada Raudhataini limeandika matukio mbalimbali ya ziara tukufu na huduma zilizo tolewa na Atabatu Abbasiyya kwa mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: