Uongozi mku wa Atabatu Abbasiyya tukufu watangaza kufaulu kwa ratiba yake ya ulinzi na utumishi kwa mazuwaru wa Shaabaniyya…

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umetangaza kufaulu kwa ratiba yake ya ulinzi na utumishi iliyo andaa kwa ajili ya mazuwaru wa Shaabaniyya, iliyo isha salama bila kutokea tatizo lolote, na kufikia malengo yake, ambayo ni kutoa huduma kwa mazuwaru na kuhakikisha wanafanya ibada ya ziara katika mazingira mazuri, mafanikio haya ni muendelezo wa mafanikio ambayo wamekua wakiyapata watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) katika shughuli zao, na mwanzo mwema wa kujiandaa kuelekea ziara zijazo.

Akaongeza kusema kua: “Hakaka mafanikio haya yametokana na ushirikiano wa watumishi wote wa Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na wafanya kazi wa kujitolea, bila kusahau ushirikiano wa hali ya juu uliopo baina yao na watumishi wa Atabatu Husseiniyya pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama vya mkoa wa Karbala, wanamchango mkubwa sana wa kuhakikisha amani na utulivu na kuwezesha utoaji wa huduma bora, pamoja na ushirikiano wa mazuwaru watukufu, wote hao wameisaidia Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia watumishi wake iweze kutoa huduma bora”.

Akamaliza kwa kusema: “Tunatoa shukrani za dhati kwa vyombo vyote vya usalama na watumishi wa Ataba zote za Karbala pamoja na wahudumu wa mawakibu (vikundi) vya Husseiniyya walio enea kila sehemu ndani na nje ya mji wa Karbala, bila kuwasahau watendaji wa serikali, wote kwa pamoja wamefanya kazi kubwa ya kufanikisha ziara hii na kuondoa kila aina ya vikwazo kwa mazuwaru”.

Kumbuka kua Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya na maeneo mengine, baada ya Adhuhuri ya jana zilifurika mamilioni ya watu waliokuja kufanya ziara ya Shaabaniyya tukufu kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala, wakiwemo mazuwaru kutoka katika nchi za kiarabua na kiajemi, ilianza kushuhudiwa idadi kubwa ya watu baada ya swala ya Dhuhuraini hadi karibu na swala ya Maghribaini na kuendelea, chini ya ulinzi mkali wa na huduma bora zilizo kua zikitolewa na watumishi wa Ataba mbili tukufu pamoja na kitengo kinacho simamia eneo la katikati ya haram mbili tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: